• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 1:14 PM
Wakufunzi Mikel Arteta na Jonas Eidevall watia saini kandarasi mpya kambini mwa Arsenal

Wakufunzi Mikel Arteta na Jonas Eidevall watia saini kandarasi mpya kambini mwa Arsenal

NA MASHIRIKA

KOCHA Mikel Arteta wa timu ya wanaume kambini mwa Arsenal na mwenzake Jonas Eidevall wa kikosi cha wanawake, wametia saini kandarasi mpya.

Arteta alipokezwa mikoba ya Arsenal mnamo Disemba 2019 na sasa amerefusha muda wa kuhudumu kwake uwanjani Emirates hadi mwishoni mwa msimu wa 2024-25.

Eidevall alijiunga na Arsenal mwishoni mwa msimu wa 2020-21 na sasa atadhibiti mikoba ya vipusa wa kikosi hicho hadi msimu wa 2023-24.

Mkurugenzi wa Arsenal, Josh Kroenke ambaye babake Stan ndiye mmiliki wa klabu hiyo, amesema mikataba mipya ambayo imetolewa kwa Arteta na Eidevall itachangia “uthabiti na kuleta mwanga zaidi katika siku za halafu”.

Kufikia sasa, Arteta ameongoza Arsenal kutinga nafasi ya nne kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kadri wanavyofukuzia nafasi ya kushiriki soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao.

Chini ya Eidevall, Arsenal wanafukuzia taji la Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake nchini Uingereza (WSL) na kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili jedwalini kwa alama moja nyuma ya viongozi na mabingwa watetezi Chelsea.

TAFSIRI: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

AS Roma yazamisha Leicester City na kutinga fainali ya...

Watu 8 waorodheshwa kupigwa msasa kubaini anayefaa kuwa...

T L