• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 12:36 PM
Wamiliki wa Inter Milan wafunga kikosi cha Jiangsu FC

Wamiliki wa Inter Milan wafunga kikosi cha Jiangsu FC

Na MASHIRIKA

WAMILIKI wa Jiangsu FC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya China (Chinese Super League), wamekifunga kikosi hicho.

Kwa mujibu wa mabwanyenye hao ambao pia wanamiliki kikosi cha Inter kinachoshiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A), maamuzi yao yalichochewa na haja ya kumakinikia biashara nyinginezo baada ya mazingira ya kuendesha soka nchini China kuwa mabovu.

Jiangsu walitawazwa wafalme wa Chinese Super League kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 2020. Hata hivyo, wamekuwa na ugumu wa kuendesha shughuli nyingi za kikosi pamoja na kumudu mishahara ya wachezaji kutokana na gharama ya juu ya matumizi ya fedha.

Hii ni baada ya mkataba wao wa Sh78 bilioni kuonyesha mechi za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) moja kwa moja nchini China kati ya 2021 na 2022 kufutiliwa mbali.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Fabio Capello aliwahi kuwa kocha wa kikosi hicho kati ya 2017 na 2018 huku mwanasoka wa Real Madrid, Gareth Bale akiwa pua na mdomo kuingia katika sajili rasmi ya Jiangsu mnamo 2019. Bale ambaye ni raia wa Wales, alirejea Tottenham Hotspur kwa mkopo mwanzoni mwa msimu huu chini ya kocha Jose Mourinho.

Kwa mujibu wa magazeti mengi nchini Italia, huenda kikosi cha Inter kikapata mmiliki mpya kufikia mwisho wa msimu huu.

Huenda maamuzi ya kufunga shughuli za Jiangsu pamoja na kubadilisha wamiliki wa Inter yakachochea pia mabadiliko kambini mwa West Bromwich Albion na Wolves – vikosi vya EPL vinavyomilikiwa na Wachina.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

AC Milan wapepeta AS Roma

Klopp adai Liverpool yaweza kufanya makuu ligini licha ya...