• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Wanasoka 6 wa Ganze wafanyiwa majaribio na klabu za Mombasa

Wanasoka 6 wa Ganze wafanyiwa majaribio na klabu za Mombasa

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

WANASOKA sita kutoka Ganze, Kaunti ya Kilifi wanaanza majaribio na klabu ya Supaligi ya Taifa ya Modern Coast Rangers FC inayotaka kuimarisha kikosi chake baada ya timu hiyo kuanza vibaya katika ligi hiyo.

Wanasoka hao, Ramadhan Luwali, Samuel Menza, Edward Khamisi (Umeme United FC), Samson Juma (Yanga Stars), Juma Charo (Majengo FC) na Kazungu Karisa (The New Saints) pia wanatarajia kufanya na Bandari Youth huku makocha wa Congo Boys wakiwakodolea macho.

Wachezaji hao walitembelea uwanja wa Serani Sports ambao unaotumiwa na Congo Boys na ambao hapo kale ulikuwa uwanja wa mazoezi wa klabu iliyokuwa maarufu zaidi kuwahi kutokea katika jimbo la Pwani ya Mwenge (Liverpool).

Mwenyekiti wa Congo Boys FC, Alamin Ahmed aliwaambia vijana hao wafanye bidii katika majaribio hayo ili wafuzu kusajiliwa na mojawapo ya klabu hizo za Modern Coast ama Bandari Youth ambayo hupandisha wanasoka wake wazuri hadi timu ya Ligi Kuu ya Kenya ya Bandari FC.

“Makocha wetu watafika kwenye viwanja vya Refinery ambako Modern Coast wanafanya mazoezi na uwanja wa Mbaraki Sports Club kuwaona ili tuone nani ataweza kutufaa nasi tuweze kumsajili,” akasema Ahmed.

Ziara ya wachezaji hao ilitokana na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Bandari FC, Twahir Muhiddin alkiyevutiwa nao wakati wa mechi za fainali za mashindano ya Chief Ken Tungule Cup zilizochezwa huko Ganze. Aliyelipia gharama za kufika Mombasa ni Mstahiki Mungela.

You can share this post!

Ongwae asalia nje Bungei aking’ara katika ushindi wa...

FIFA yampiga Cavani marufuku ya mechi mbili za kimataifa...