• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 PM
Wanyama mawindoni Klabu Bingwa CONCACAF

Wanyama mawindoni Klabu Bingwa CONCACAF

Na GEOFFREY ANENE

CF Montreal anayochezea Mkenya Victor Wanyama itajibwaga uwanjani Azteca nchini Mexico kuzichapa dhidi ya wenyeji Cruz Azul katika mechi ya mkondo wa kwanza ya robo-fainali ya Klabu Bingwa ya Amerika Kaskazini, Kati na Carribean (CONCACAF) mapema Alhamisi.

Montreal ya kocha Wilfried Nancy itahitaji kujikakamua zaidi kwa sababu inachechemea kwenye Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS). Ilifungua msimu wa MLS kwa kuchapwa na Orlando City 2-0 na Philadelphia Union 2-1.

Ilijikatia tiketi ya robo-fainali ya CONCACAF baada ya kuduwaza Santos Laguna kutoka Mexico 3-0 nchini Canada katika mechi ya marudiano ya 16-bora ambapo ilikuwa imeanza vibaya kwa kupigwa ugenini 1-0.

Cruz Azul pia inapitia ugumu kwenye Ligi Kuu ya Mexico ambapo imekamilisha michuano mitatu mfululizo ushindi.

“Tunajua kuwa kuna wakati mgumu tutapitia na pia tunafahamu kuwa mechi dhidi ya timu kutoka Mexico huwa si rahisi. Lazima tucheze mchezo wetu na pia kujituma vilivyo kupata matokeo mazuri,” alisema kocha Mfaransa, Nancy.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza, Montreal itakosa huduma za mshambulizi matata Romell Quioto aliyelishwa kadi mbili za njano katika raundi ya 16-bora.

Montreal itaalika Cruz Azul uwanjani Olympic kwa mechi ya marudiano mnamo Machi 16

  • Tags

You can share this post!

Marjan ateuliwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC

KAULI YA WALLAH BIN WALLAH: Ukijiamini na uzingatie...

T L