• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Winavishale wa Bode la Ufa wahifadhi taji la Inter Prisons

Winavishale wa Bode la Ufa wahifadhi taji la Inter Prisons

Na JOHN KIMWERE

NAHODHA wa timu ya vishale ya Mkoa wa Bode la Ufa (Rift Valley), Wilson Chumek amepongeza wachezaji wake baada ya kujituma kwa udi na uvumba na kuhifadhi taji la Inter Prisons kwenye michezo iliyoandaliwa Kamiti Prisons, Kiambu. ”Nashukuru wenzangu kwa kuonyesha mchezo mzuri na kuibuka mabingwa kwa mara ya pili,” alisema na kuongeza kuwa kamwe haikuwa rahisi.

Timu ya Bode la Ufa iliibuka mabingwa kwa kuzoa jumla ya pointi 102, 11 mbele ya Nairobi na Mashariki. Katika fainali, Bode la Ufa walizoa alama 19-8 dhidi ya Nairobi. Kwenye nusu fainali, Bode la Ufa ilishinda Mkoa wa Kati kwa alama 19-9 nayo Nairobi ilizaba Mkoa wa Mashariki kwa alama 19-13.

Kwenye mechi za kitengo cha mchezaji mmoja mmoja (singles) kitengo cha wanaume, Wilson Chemuk wa Bode la Ufa aliibuka bingwa naye Peter Ngari wa Nairobi alimaliza namba mbili baada ya kushinda mechi 48 na 46 mtawalia kati ya mechi 64 walizocheza. Kitengo cha wanawake, Ann Machira wa Nairobi aliibuka bingwa aliposhinda mechi 32- 17 dhidi ya mwenzake Risper Kurgat.

Timu ya Mkoa wa Pwani iliyomaliza ya sita pia ilituzwa kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kwenye mashindano hayo.

  • Tags

You can share this post!

Base Titanium yasifiwa kwa kuwezesha jamii

Bonyeza *106# kuthibitisha kama laini yako imesajiliwa...

T L