• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Wolves wamsajili beki mzoefu Craig Dawson kutoka West Ham United

Wolves wamsajili beki mzoefu Craig Dawson kutoka West Ham United

Na MASHIRIKA

WOLVERHAMPTON Wanderers wamejinasia huduma za beki mzoefu Craig Dawson kutoka West Ham United kwa Sh508 milioni.

Difenda huyo raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 32 anaingia katika sajili rasmi ya Wolves baada ya kutia saini mkataba wa miaka miwili na nusu.

Anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Wolves mwezi huu wa Januari 2023 baada ya kocha mpya Julen Lopetegui kujinasia pia maarifa ya kiungo Mario Lemina, winga Pablo Sarabia na fowadi Matheus Cunha.

Beki huyo wa zamani wa West Bromwich Albion amewajibishwa katika mechi 246 za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na amekuwa mchezaji wa West Ham kwa kipindi cha misimu miwili iliyopita.

Wolves ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya 17 kwenye msimamo wa jedwali la EPL, watakuwa wageni wa Manchester City katika kipute hicho mnamo Januari 22, 2023 ugani Etihad.

Mechi ya mwisho ambayo Dawson alichezea West Ham ilikuwa iliyowashuhudia wakikomoa Brentford katika Kombe la FA mnamo Januari 7, 2023. Nyota huyo hakusajiliwa kwa wakati ufaao ndipo aweze kuwajibishwa dhidi ya Man-City.

Aliingia mwanzo kambini mwa West Ham kwa mkopo kutoka Watford mnamo Oktoba 2020 kabla ya kupokezwa mkataba wa kudumu. Alichezea West Ham katika mechi 87 na akafunga mabao matano katika michuano yote.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

DARUBINI YA WIKI: Toleo Nambari 21 | Januari 22, 2022

Kocha Frank Lampard katika hatari ya kutimuliwa ugani...

T L