• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Xhaka amjeruhi Lacazette wakiwa mazoezini kambini mwa Arsenal

Xhaka amjeruhi Lacazette wakiwa mazoezini kambini mwa Arsenal

Na MASHIRIKA

ALEXANDRE Lacazette ameonya kwamba huenda akakosa mchuano wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kati yao na Leeds United mnamo Februari 14, 2021 uwanjani Emirates baada ya kuumizwa na kiungo Granit Xhaka wakishiriki mazoezi ya pamoja Ijumaa jioni.

Nyota huyo raia wa Ufaransa alitumia mtandao wake wa Instagram kuanika kiwango cha jinsi alivyojeruhiwa na Xhaka mguuni.

“Jeraha kwa hisani ya Granit Xhaka! Nilidhani sisi ni marafiki, kumbe sivyo!” akasema Lacazette katika ujumbe ulioibua utani mkubwa miongoni mwa mashabiki wa Arsenal mtandaoni.

Lacazette, 29, alitarajiwa kuongoza safu ya mbele ya Arsenal dhidi ya Leeds United ikizingatiwa kusuasua kwa nahodha Pierre-Emerick Aubameyang ambaye hajarejelea ubora aliokuwa akijivunia ndani ya jezi za Arsenal katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita.

Lacazette ambaye ni mchezaji wa zamani wa Olympique Lyon nchini Ufaransa, angali na mkataba wa mwaka mmoja pekee kambini mwa Arsenal na tayari anahusishwa na uwezekano mkubwa wa kuyoyomea Uhispania kuvalia jezi za Barcelona wanaonolewa na kocha Ronald Koeman.

Maarifa ya Lacazette yanawaniwa pia na Real Madrid ambao ni watani wakubwa wa Barcelona katika soka ya Uhispania (La Liga). Vikosi vingine vinavyohemea huduma za Lacazette ni Atletico Madrid kutoka Uhispania na Juventus ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Chini ya kocha Mikel Arteta, Arsenal watakosa pia maarifa ya beki Kieran Tierney na kiungo Thomas Partey dhidi ya Leeds United baada ya sogora huyo raia wa Ghana kupata jeraha wikendi iliyopita dhidi ya Aston Villa kwenye gozi la EPL.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

AKILIMALI: Mfumo wa Hydroponic na mbinu asilia kukabili...

AUSTRALIAN OPEN: Mwanatenisi Medvedev atoka nyuma na...