• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 5:55 AM
Zetech Sparks yasajili watano

Zetech Sparks yasajili watano

NA RUTH AREGE

TIMU ya Zetech Sparks ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL), imesajili wachezaji watano wapya ikiwa ni kujiandaa kwa msimu wa 2022/23 ambao haujulikani utaanza lini.

Kipa Monicah Karambu amejiunga na klabu hiyo akitokea Thika Queens, beki wa kati Shelyn Mbuto amesajiliwa kutoka Shule ya Upili ya Wasichana ya Kilimo kutoka Kakamega.

Kiungo Susan Nyumba naye ni wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Nyakach.

Mshambuliaji Pauline Aisu ametokea Kisumu All Starlets ya KPWL naye kiungo Maurine Aringo amesajiliwa akitokea Uweza Women ya Ligi ya Taifa ya Divisheni ya Kwanza.

Wakati huo huo, Sparks wameachilia Lydia Akoth, Valentine Kwaka na Phoskah Nashivanda ambao wamejiunga na Gapso Women ya KWPL naye Joy Kinglady alijiunga na wanajeshi wa Ulinzi Starlets.

Kulingana na kocha wa klabu hiyo Bernard Kitolo anasema sasa Sparks ina kikosi madhubuti.

“Wachezaji wazuri wameondoka kwenye timu na kuacha chipukizi. Sajili ambazo nimefanya ni za kukiimarisha kikosi. Wachezaji hao wageni wana uzoefu wa kucheza kwenye ligi. Msimu ujao, kutakuwa na ushindani mkubwa kwenye nafasi ya kati. Sitaki makosa ambayo tulifanya msimu jana yatupate tena,” alisema Kitolo.

Kuhusiana na kucheza ligi ambayo inaendeshwa na Kamati ya Mpito ya Shirikisho la Soka nchini (FKF), Kitolo anasema wako tayari kucheza chini ya yeyote yule ambaye atakuwa ofisini.

“Tunasubiri kujua mwelekeo kutoka kwa serikali. Sisi tutacheza ligi ambayo inatambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). Tumejitayarisha vilivyo na tuko tayari kupambana,” aliongezea Kitolo.

Wakati huo huo, kamati ya mpito ilitoa ratiba ya mechi za msimu mpya wa Ligi ya Wanaume nchini (KPL). Kamati hiyo imesema kuwa, msimu mpya utaanza rasmi siku ya Jumamosi wiki hii.

  • Tags

You can share this post!

Raia wa Uganda anayeshukiwa kumuua mke-mwenza ndani

Mpira wa Vikapu: Timu nne za Kenya zawinda taji la Red...

T L