• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Chama cha Kanu chazindua manifesto yenye nguzo tano kuu

Chama cha Kanu chazindua manifesto yenye nguzo tano kuu

Na CHARLES WASONGA

MWENYEKITI wa Kanu Gideon Moi amezindua manifesto ya chama hicho yenye nguzo tano za kiuchumi, ikiwemo adhabu ya kifo kwa wahalifu wa kiuchumi.

Chama hicho kinasema adhabu hiyo ni mojawapo ya mikakati yake ya kuzima ufisadi nchini.

Seneta Moi alisema Kanu imeweka ajenda yake kwa taifa hili kupitia kile anachodai ni “manifesto yenye nguzo tano za kupiga jeki biashara na kuleta mabadiliko.”

Akiongea wakati wa kuzinduliwa kwa manifesto hayo Jumatano katika Kabarnet Garden, Nairobi Bw Moi, ambaye alikuwa ameandamana na Katibu Mkuu Nick Salat na wanachama wengine, alisema chama hicho kitaendeleza nguzo tano mahususi za kustawisha Kenya.

Nguzo hizo ni; uimarishaji wa uchumi, ugatuzi, miundo msingi, upandaji miti nchini na uwajibikaji wa wananchi.

“Chini ya nguzo ya kiuchumi (uchumi na kazi) tunalenga kuimarisha sekta ya utengenezaji bidhaa, kujenga upya uchumi kuanzia mashinani katika sekta kama vile; kilimo, ufugaji, uchumbaji na kubuni nafasi za ajira,” seneta Moi akasema katika Kabarnet Garden.

Aliongeza kuwa chini ya nguzo hiyo, Kanu inalenga kuimarisha sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT), kilimo na uzalishaji chakula, fedha za umma na kupunguza mzigo wa deni la kitaifa.

“Muhimu zaidi ni kwamba tunalenga kupambana na ufisadi na wizi wa mali ya umma kwa kuanzisha adhabu ya kifo kwa watakaopatikana na hatia hiyo,” akaeleza seneta Moi.

Kuhusu ugatuzi, seneta huyo wa Baringo alisema Kanu inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma sehemu za mashinani.

  • Tags

You can share this post!

Mwanahabari Eliud Waithaka azikwa Nyandarua

Serikali yatangaza mikakati ya kuboresha sekta ya bodaboda

T L