• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 1:16 PM
Kenya Kwanza yadai bandari zote nchini zimeuzwa kwa Dubai

Kenya Kwanza yadai bandari zote nchini zimeuzwa kwa Dubai

NA LEONARD ONYANGO

MUUNGANO wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Naibu wa Rais William Ruto sasa unadai Serikali inapanga kukabidhi bandari tatu za Kenya kwa kampuni ya Uarabuni.

Kwenye taarifa iliyosomwa na Kinara wa Amani National Congress (ANC), Musalia Mudavadi, viongozi wa Kenya Kwanza walisema usimamizi wa bandari za Mombasa, Lamu na Kisumu umepeanwa kwa kampuni kutoka Milki ya Uarabuni (UAE).

Kulingana na Bw Mudavadi, hatua hiyo ni hujuma kwa usalama wa kitaifa kutokana na umuhimu wa bandari hizo kwa Kenya, akieleza kuwa Kenya haitakuwa na usemi wa bandari hizo baada ya kutwaliwa na wageni.

“Mpango huo ni haramu kwani wananchi hawakushirikishwa na ulikiuka kifungu cha 227 cha Katiba kuhusu Kandarasi za Umma,” akasema Bw Mudavadi.

Alidai kuwa serikali pia ilikosa kushirikisha Bunge kinyume na Katiba inayotaka wabunge kuhusishwa katika maamuzi muhimu.

“Kandarasi hiyo haikuidhinishwa na Baraza la Mawaziri na wala na wala serikali za kaunti hazikuhusishwa. Hata shirika la ndege likitaka kuanza safari zake nchini Kenya ni sharti lipate idhini ya Bunge kupitia kamati husika,” wakasema viongozi hao.

  • Tags

You can share this post!

Ruto akubaliana na IEBC, Raila apinga

Farm shield: Kifaa kinachorejelewa kama ubongo wa shamba

T L