• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 3:13 PM
Khalwale mfia Ruto anayeamini ataingiza Mudavadi katika Wilbaro

Khalwale mfia Ruto anayeamini ataingiza Mudavadi katika Wilbaro

Na LEONARD ONYANGO

ALIYEKUWA Seneta wa Kakamega Boni Khalwale ana sifa zote za wanasiasa wa Kenya – yaani kuwa na midomo miwili.

Miaka michache iliyopita, Bw Khalwale alikuwa mkosoaji mkuu wa Naibu wa Rais William Ruto lakini sasa yuko tayari kupigwa rungu kwa niaba ya kiongozi huyo wa chama cha United Democratic Alliance (UDA).Miezi michache kabla ya uchaguzi wa 2017, Bw Khalwale alimtaka Dkt Ruto kuelezea Wakenya mahali alipata mamilioni ya fedha ambayo amekuwa akigawa makanisani kila wiki.

“Ikiwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, atapata nafasi atauliza Naibu wa Rais Ruto kwamba mshahara unaopata hauwezi kukuwezesha kujenga nyumba ya kifahari kwa gharama ya Sh1.2 bilioni. “Mheshimiwa Ruto, mshahara ambao wewe unalipwa hauwezi kukupatia nguvu za kununua hoteli ya Dolphin Beach huko Mombasa.

Huo mshahara hauwezi kukuwezesha kununua helikopta nne,” akasema Bw Khalwale.Seneta huyo wa zamani pia alidai kuwa viongozi kutoka Magharibi waliounga mkono Ruto walipewa hongo.Lakini siku hizo Bw Khalwale amegeuka mtetezi mkuu wa Dkt Ruto na amekuwa akitumia mitandao kupigania Naibu wa Rais.

Wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge wa Kibra Novemba 2019, Bw Khalwale alifichua kuwa alilazimika kuvumilia mashambulio ya mawe kutoka kwa wafuasi wa ODM baada ya Dkt Ruto kuwaagiza wasiondoke hadi kura zitakapohesabiwa.

Mbali na kupigana, Bw Khalwale pia ameiga ujanja wa Dkt Ruto wa kula kwenye vibanda ili kuonekana mlalahoi au hasla.Alhamisi, Bw Khalwale anayemezea mate ugavana wa Kakamega, alijawa na furaha tele baada ya kinara wa Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetang’ula kukataa kuhudhuria kongamano la Azimio la Amani lililofanyika Ijumaa ambapo kiongozi wa ODM Raila Odinga alitangaza azma ya kuwania urais.

Kulingana na Khalwale, hatua ya Bw Mudavadi na Bw Wetang’ula kukataa kuhudhuria kongamano la Azimio la Umoja ni ishara kwamba wawili hao wanaelekea kwa Dkt Ruto.

You can share this post!

Jamhuri ya mwisho ya Uhuru

Wandani wa Ruto: Raila atasalitiwa

T L