• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 3:21 PM
Kumzuilia Ruto ni sawa na jinsi Miguna alihangaishwa, adai Murkomen

Kumzuilia Ruto ni sawa na jinsi Miguna alihangaishwa, adai Murkomen

Na WINNIE ONYANDO

KUZUILIWA kwa Naibu Rais Dkt William Ruto Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) kusafiri kwenda Uganda kumewakera wandani wake.

Dkt Ruto alipanga kuzuru nchi hiyo jirani jana lakini maafisa wa Idara ya Uhamiaji walimzuilia wakidai kuwa anahitajika kupata idhini ya kutoka nje ya nchi kutika Afisi ya Rais.

Naibi Rais hajawahi kuhitaji idhini yoyote ya kusafiri nje ya nchi hapo awali. Mwandani wake mkuu wa kisiasa, seneta wa Elgeyo- Marakwet Kipchumba Murkomen amefananisha tukio hilo na mahangaiko  Dkt Miguna Miguna alipitia.

“Dkt Ruto hajawahi kuhitaji idhini yoyote ya kusafiri nje ya nchi. Hakuna sheria yoyote inayomhitaji kupewa ruhusa akitaka kufanya ziara ya kibinafsi. Kilichofanyika leo ni kumkosea heshima Naibu Rais,” alisema Bw Murkomen katika akaunti yake ya Twitter.

Mbunge wa Kiharu, Bw Ndindi Nyoro naye alitaja tukio hilo kama aibu kwa kiongozi wao huku akiisuta serikali kwa kumnyima Dkt Ruto idhini ya kufanya ziara zake za kibinafsi.

“Sijawahi kuona aibu kama hii. Inakuaje Afisi ya Rais inakataa kumpa idhini Naibu Rais wa nchi?” Bw Nyoro aliteta.

Afisi ya Dkt Ruto nayo ililalama ikisema kuwa: “Hata kama Rais hampendi Dkt Ruto, basi anapaswa kuheshimu ofisi yake kama Naibu Rais kwa kuwa wote walichaguliwa na wananchi.”

Haya yanajiri baada ya kiongozi huyo kusafiri nchi hiyo mwezi jana kwa shughuli ambazo hazikuelezwa.

 

You can share this post!

Sababu zilizofanya chama cha Jubilee kusambaratika

Msaka kazi ashtakiwa kuwapora wanabenki watatu Sh255,000...