• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Mlinzi wa Malala akamatwa kwa kufyatua risasi hewani

Mlinzi wa Malala akamatwa kwa kufyatua risasi hewani

Na SAMMY WAWERU

Mlinzi wa Seneta wa Kakamega, Bw Cleophas Malala amekamatwa Alhamisi na maafisa wa polisi katika eneo la Matungu kwa kile idara ya polisi imehoji “ametumia vibaya silaha yake”.

Mlinzi wa seneta huyo anasemekana kufyatua risasi hewani ili kufurusha kundi la vijana waliotaka kuteketeza gari la Bw Malala, kufuatia vurumai na vurugu zilizozuka wakati wa uchaguzi mdogo eneobunge la Matungu.

Kwenye video inayosambaa mitandaoni, mlinzi huyo wa kiume anaonekana akitiwa nguvuni na maafisa wa usalama, wanaojumuisha wale wa kutoka kikosi cha kukabiliana na ghasia (GSU).

“Weka yeye kwenye gari…” afisa mmoja wa polisi anaskika akisema, huku akimshika mashati.

Mchana kutwa, seneta Malala alizua ubishi mkali katika mojawapo ya kituo cha kupigia kura Matungu, kwa kile alidai “kulikuwa na njama ya wizi wa kura iliyotekelezwa na chama cha ODM”.

Malala amesema chama cha ANC na ambacho kinaongozwa na Bw Musalia Mudavadi hakitakubali matokeo ya uchaguzi huo mdogo, alioshikilia umekumbwa na udanganyifu wa kura.

Huku shughuli za kuhesabu kura zikiendelea, ushindani mkali unatarajiwa kushuhudiwa kati ya Mabw Alex Lanya wa UDA, Paul Were (ODM) na Oscar Nabulindo (ANC).

You can share this post!

Sonko anaugua maradhi ya ubongo na moyo, hawezi kuendelea...

Malala na Echesa mafichoni wakisakwa na polisi kwa kuzua...