• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Mshangao jina la Ngilu kuwa debeni

Mshangao jina la Ngilu kuwa debeni

NA KITAVI MUTUA

JINA la Gavana wa Kitui Charity Ngilu ambaye alijiondoa katika kinyang’anyiro cha Ugavana, jana Jumanne lilikuwa kwenye karatasi ya kupiga kura licha ya kujiondoa mwezi Julai.

Bi Ngilu alisema kuwa aliarifu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) iondoe jina lake kutoka kwa wawaniaji wa ugavana mnamo Julai 19.

“Nilitarajia kuwa IEBC ingechukua hatua na kuliondoa jina langu baada ya kuwaandikia. Makosa hayo hayangetokea kwa sababu yatasababisha kura nyingi zipotee,” akasema.

“Watu wa Kitui wanajua kuwa nilikuwa namuunga mkono David Musila na hilo halijabadilika,” akaongeza.

Bi Ngilu alitangaza kuwa amejiondoa katika kutetea kiti chake wakati Mwaniaji wa Urais wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga alipoandaa mkutano mkubwa wa kisiasa katika soko la Mutha, eneobunge la Kitui Kusini mnamo Juni 15.

Wakati wa mkutano huo, Bw Odinga aliahidi kumtunuku Bi Ngilu ambaye ni kiongozi wa Narc wadhifa muhimu ndani ya serikali yake akishinda Urais.

Hii ilikuwa mara ya kwanza ndani ya miaka 30 na chaguzi saba ambapo Bi Ngilu hakuwa akiwania cheo chochote kisiasa.

  • Tags

You can share this post!

Wachache wajitokeza kupiga kura Thika na Ruiru

ODM yashuku hila ugavana ukiahirishwa

T L