• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
PAA yajitenga na ziara ya Raila Pwani

PAA yajitenga na ziara ya Raila Pwani

Na CHARLES WASONGA

MGAWANYIKO umetoa ndani ya vuguvugu la Azimio la Umoja baada ya chama cha Pan African Alliance (PAA) kutangaza kuwa hakitashiriki katika mikutano ya kampeni itakayoongozwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga eneo la Pwani.

Kiongozi wa chama hicho Gavana wa Kilifi Amason Kingi alisema wameamua kujiondoa kutoka shughuli za ziara hiyo baada ya viongozi wa ODM kutoka Pwani kudai “ni shughuli ya ODM pekee”

“Awali tuliambiwa kuwa kamati andalizi ya kampeni hiyo itajumuisha wanachama kutoka vyama vyote chini ya mwavuli wa Azimio la Umoja. Lakini viongozi wa ODM wamesisitiza kuwa shughuli hiyo ni yao. Kwa hivyo, PAA haitashiki katika mikutano iliyoandaliwa na chama kimoja katika vuguvugu la Azimio la Umoja,” Bw Kingi akasema kwenye taarifa Ijumaa, Februari 18, 2022.

Bw Odinga anaanza ziara yake ya kaunti za Mombasa, Kilifi, Kwale na Taita Taveta Jumamosi, Februari 19, 2022 siku moja baada kuwasili nchini kutoka ziara nchini Ethiopia, India na Dunia.

Hata hivyo, Gavana Kingi ambaye alichaguliwa kwa tiketi ya chama cha ODM, kabla ya kukosana na uongozi wake, alisema PAA itaendelea kumuunga Bw Odinga na Azimio la Umoja.

“Bado tunaunga mkono sera za Azimio la Umoja ambazo zinaendeleza umoja wa kitaifa pasina vigezo vya kidini na kisiasa,” akasema.

You can share this post!

Buriram yafungua mwanya wa alama 10 Ligi Kuu ya Thailand

UhuRuto wachoma mabilioni ya miradi

T L