• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Raila amgonga Ruto kwenye kampeni Pwani

Raila amgonga Ruto kwenye kampeni Pwani

NA WAANDISHI WETU

KINARA wa ODM Raila Odinga, amemtaja Naibu Rais Dkt William Ruto kama kiongozi ambaye amezoea kuhadaa Wakenya ili kupata ufuasi hasa uchaguzi mkuu Agosti 9 unapokaribia.

Bw Odinga aliwataka Wakenya wasiamini ahadi ambazo Dkt Ruto anatoa kwenye mikutano yake akisema kuwa baadhi ya miradi aliyoahidi katika mwaka wa 2013 haijatekelezwa hadi sasa.

“Jina jingine la Ruto ni Bw Ahadi. Aliwaambia mnamo 2013 kuwa kila mtoto shuleni chini ya miezi sita atakuwa na kipakatalishi. Alitoa ahadi hiyo na hajaitimiza ilhali sasa anawapa wanafunzi hao ambao sasa wanamaliza masomo ya shule ya sekondari wilbaro,” akasema Bw Odinga.

Bw Odinga alikuwa akihutubu kwenye mkutano wa kisiasa katika wadi ya Bamba eneobunge la Ganze, Kaunti ya Kilifi katika siku ya kwanza ya zi – ara yake ukanda wa Pwani.

“Ruto alisema kila kaunti itakuwa na uwanja wa michezo. Hapa Kilifi mmepata uwan – ja wowote? Aliahidi vijana milioni

moja ajira akashindwa kuitekeleza na sasa anaahidi nafasi milioni nne baada ya kusahau kuwa alishindwa kutekeleza ile ya kwanza,” akaongeza waziri huyo mkuu wa zamani.

Kauli yake inakuja wakati ambapo Naibu Rais amekuwa akimwelekezea cheche kali Rais Uhuru Kenyatta akimlaumu kwa kumtenga na ufanisi wa utawala wa Jubilee. Alimlaumu kiongozi wa nchi “kwa kupotoshwa na Bw Odinga” hadi akashindwa kutekeleza ajenda za serikali.

Kwenye kampeni yake katika Kaunti ya Kiambu mnamo Ijumaa, Dkt Ruto alidai kuwa walitekeleza ahadi nyingi katika muhula wao wa kwanza ila mambo yakatumbukia nyongo baada ya Rais Kenyatta kuingia kwenye ushirikiano na Bw Odinga kupita handisheki mnamo Machi, 2018.

Hata hivyo, Bw Odinga alimpuuza Dkt Ruto akisema kuwa yeye ni naibu rais na kupitia mamlaka yake, ana uwezo wa kutekeleza ahadi tele alizotoa.

Kinara huyo wa ODM lipuuza madai kuwa yeye ni mradi wa serikali, akisema ni mwanasiasa mwenye historia pevu ambaye amekuwa akijisimamia kisiasa kwa miaka mingi.

“Nilishindana nao 2013, na baada ya kura ya 2017, nikaelekea mahakamani kisha ikathibitishwa kura ziliibwa. Mkiniona, mimi niliyehudumu kama waziri mkuu na kuwa katika siasa miaka hii yote ninaweza kuwa mradi wa mtu?” akauliza Bw Odinga.

Katika kesi aliyopinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2017, mahakama ilisema mipangilio ya uchaguzi haikufuatwa kikamilifu ili kuweza kupata matokeo ya kuaminika.

Mbunge huyo wa zamani wa Lang’ata aliahidi kutatua masuala ya ardhi Pwani na pia tatizo la tangu kale la ukosefu wa maji.

Bw Odinga alikuwa ameandamana na Gavana wa Mombasa Hassan Joho, Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo, Naibu Gavana wa Kilifi Gideon Saburi, mbunge wa Ganze Teddy Mwambire na wanasiasa wengine. Aliwapokea mawaziri wasaizidi wa zamani Harrison Kombe, Francis Baya pamoja na wanasiasa wengine ambao walihama mrengo wa UDA na kujiunga na ODM.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru aanza kutoa Jubilee ICU

Kenya yatahadhari polio ikigunduliwa Malawi

T L