• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Raila arai wakazi wa Mlima Kenya kwa kuahidi kuimarisha kilimo

Raila arai wakazi wa Mlima Kenya kwa kuahidi kuimarisha kilimo

NA IRENE MUGO

MWANIAJI urais wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga, Jumapili alirai wapigakura wa eneo la Mlima Kenya akiahidi kuimarisha uchumi, kujenga barabara na kuwasaidia wakulima.

Bw Odinga alisema iwapo atatwaa uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, atapunguza bei ya mbolea, pembejeo za kilimo na kuhakikisha kuna soko la kuuza bidhaa.

“Kupitia uimarishaji kilimo, wakulima watapata faida kubwa na kutajirika,” alisema Bw Odinga.

Waziri huyo mkuu wa zamani alisema serikali yake itahakikisha elimu ya bure itaanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Akihutubia halaiki kubwa ya wakazi baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa la St Peter ACK, Nyeri, Bw Odinga alikosoa kampeni za Naibu wa Rais William Ruto za mfumo wa kukuza uchumi kutoka mashinani, akidai hauwezi kufaulu lakini.

“Tunataka vijana wetu wawe na pesa za kujiimarisha na kuwasaidia wazazi wao. Mikopo itatolewa kwa wale wanaotaka kuanzisha biashara,” akasema Bw Odinga.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yaagiza shule kufunguliwa Baringo

Harmonize motoni Nairobi kwa kukosa kuimba vilabuni

T L