• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Raila atashinda urais kwa asilimia 60 – Peter Kenneth

Raila atashinda urais kwa asilimia 60 – Peter Kenneth

NA MWANDISHI WETU

MWANIAJI URAIS WA muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga, atashinda urais kwa kati ya asilimia 60 na 65 iwapo wapigakura katika ngome zake watajitokeza kwa wingi kumchagua kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kenneth amesema.

Mwanasiasa huyo am – baye ni mmoja wa viongo – zi wanaopigiwa upatu kuwa mgombea mwenza wa Bw Odinga, anasema kwamba waziri mkuu huyo wa zamani amedumisha umaarufu katika ngome zake, jambo linalomweka kifua mbele kwenye uchaguzi mkuu ujao.

“Raila atashinda urais kwa asilimia 60 na 65 hivi. Hii itategemea idadi ya wapigakura watakaojitokeza katika ngome zake za jadi na zile mpya. Ninasema haya kwa sababu ukiangalia eneo la Nyanza liko

nyuma yake kama zamani na atapata kura nyingi,” alisema Bw Kenneth kwenye mahojiano na Taifa Jumapili.

Alisema amezuru eneo la Magharibi mwa Kenya akiwa na Bw Odinga kufanya kampeni na kuamini kuwa kiongozi huyo wa chama cha ODM angali maarufu eneo hilo.

“Raila huwa maarufu eneo la Nairobi licha ya chaguzi kali za awali. Sio siri kwamba ana wafuasi wengi eneo la Pwani.

Ukiangalia eneo la Mashariki, anaungwa mkono na viongozi wengi wa eneo hilo huku Marsabit na Isiolo zikiunga Raila wakiwemo magavana wa zamani na wanaohudumu kwa sasa,” akasema Bw Kenneth.

Kulingana na Bw Kenneth, Azimio itakuwa na wagombeaji katika kaunti za West Pokot, Turkana, Samburu, Nakuru, Narok na Kajiado, hatua ambayo itamfanya Bw Odinga kuzoa

kura katika eneo la Rift Val – ley, ngome ya Naibu Rais William Ruto.

“Raila anaweza kupata kati ya asilimia 30 na 40 katika eneo la Rift Valley. Hii inaacha eneo la Mlima Kenya na Kati ambako hajawahi kupata zaidi ya asilimia tano. Ninaweza kukuhakikishia kwam – ba tunapoongea sasa, hayuko katika asilimia tano bali anaweza kupata zaidi. Nafikiri kati ya asilimia 30 na 40 na ninaamini uchaguzi unapokaribia, umaarufu wake utaongezeka na kumwezesha kupata zaidi ya 50 katika eneo la Kati ya Kenya na hii inanifanya kuamini kwamba atashinda kwa kati ya asilimia 60 na 65,” akasema Bw Kenneth.

Mwanasiasa huyo alisema kwamba iwapo wafuasi wa Bw Odinga watajitokeza kupiga kura kwa wingi Agosti 9, uchaguzi wa urais utaamuliwa katika raundi moja tu.

“Huu utakuwa ushindi wa wazi. Raila atashinda katika raundi ya kwanza,” alisema.

Bw Kenneth ni mmoja wa wanasiasa ambao wamekuwa wakimpigia debe Bw Odinga katika eneo la Mlima Kenya.

Aligombea ugavana katika Kaunti ya Nairobi kwenye uchaguzi mkuu wa 2017 lakini akashindwa na aliyekuwa gavana Mike Sonko.

  • Tags

You can share this post!

Umaarufu wa UDA kwenye ngome kuu watiliwa shaka

Wanjigi adai Raila ni kivuli cha Uhuru

T L