• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 AM
Wanjigi adai Raila ni kivuli cha Uhuru

Wanjigi adai Raila ni kivuli cha Uhuru

NA MAUREEN ONGALA

MGOMBEA URAIS WA chama cha Safina, Jimmy Wanjigi, amemuonya Rais Uhuru Kenyatta dhidi ya kuingilia uchaguzi mkuu wa Agosti 9 akisema anafaa kustaafu kwa amani baada ya kuhudumu kwa vipindi viwili.

Akizungumza mjini Malindi katika kikao na wawakilishi wa jamii za Gema, Bw Wanjigi alisema Rais Kenyatta anatumia muungano wa Azimio la Umoja One Kenya kwa maslahi yake binafsi wala sio kwa manufaa ya Wakenya.

Alisema hatua ya Rais Kenyatta kuwa mwenyekiti wa Baraza la Muungano

wa Azimio ni ishara kuwa bado ana tamaa ya uongozi nchini hata baada ya kutoka mamlakani.

“Rais anajaribu kuendelea kuwa rais kinyume cha sheria na katiba ya Kenya. Tumeona makubaliano ya muungano wa Azimio ambapo rais Uhuru ndiye kiongozi wao.Kikatiba anastahili kustaafu Agosti 9 mwaka huu lakini ana mpango wa kufanya Kenya kuwa nchi ya kikomunisti,” akasema.

Bw Wanjigi aliwatahadharisha Wakenya kuwa makini na kusema kuwa sio kinara wa ODM Raila Odinga anayegombea urais kwa tikiti ya Azimio bali ni Rais Kenyatta.

“ Ninataka kumwambia Rais Kenyatta aende nyumbani, alipewa miaka 10 ya uongozi na hatutaki kumuona tena,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Raila atashinda urais kwa asilimia 60 – Peter Kenneth

Keter akubali kushindwa na limbukeni wa siasa

T L