• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Ruto awanyonga Musalia, Wetangula

Ruto awanyonga Musalia, Wetangula

NA MARY WANGARI

VYAMA vikuu vya kisiasa eneo la Magharibi mwa Kenya vya Amani National Congress (ANC) cha Musalia Mudavadi na Ford Kenya chake Moses Wetangula vimeonekana kupoteza umaarufu baada ya United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais William Ruto kuthamini wagombezi kupambana navyo.

Katika Kaunti ya Vihiga inayochukuliwa kuwa ngome kuu kisiasa ya Bw Mudavadi, wagombea watatu wamejitokeza kuwania nyadhifa. Hao ni pamoja na Yusuf Chanzu anayemezea mate kiti cha eneobunge la Vihiga, Tom Atingo anayetaka ubunge Luanda na Bi Jackline Mwenesi anayewania kuwa Mwakilishi Mwanamke wa kaunti hiyo.

Katika Kaunti ya Kakamega, wagombea kadhaa wanamezea mate viti mbalimbali kwa kutumia tiketi ya UDA akiwemo Seneta wa zamani Bonni Khalwale.

Katika nyadhifa za ubunge, Paul Posho anataka kiti cha eneobunge la Matungu naye Stanley Waiswa kiti cha Navakholo kwa UDA.

UDA pia inatazamiwa kuteua atakayegombea kiti cha Mwakilishi Mwanamke Kakamega baina ya wagombea wake watatu waliojitokeza ambao ni pamoja na Penina Mukabane, Hadija Nganyi na Mercy Luseno.

Chama hicho cha Dkt Ruto pia kinasubiriwa kutaja wagombea wake katika maeneobunge 10 ya Kakamega.

Ford Kenya inawakilishwa na mgombea mmoja pekee katika Kaunti ya Bungoma ambaye ni Spika wa Seneti Kenneth Lusaka anayewania ugavana.

Katika Kaunti ya Trans Nzoia, UDA imeonekana kutamba huku mgombea wake Philemon Samoei anayewania kwa tiketi ya UDA akitazamiwa kumenyana na mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa anayemezea ugavana kwa tiketi ya Ford Kenya.

Hali hii imezua tumbojoto huku wafuasi wa ANC wakihofia kupoteza idadi kubwa ya viti kwa vyama vinginevyo ikiwemo UDA.

  • Tags

You can share this post!

LEONARD ONYANGO: Kaunti zilinde vyanzo vya maji mijini kwa...

Ahadi ya Uhuru kuhusu stima yakosa kutimia

T L