• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Rutto aonya ugatuzi utafeli kabisa iwapo mbinu zake hazitazingatiwa

Rutto aonya ugatuzi utafeli kabisa iwapo mbinu zake hazitazingatiwa

Na KNA

ALIYEKUWA gavana wa Bomet, Bw Isaac Rutto, amedai kuwa ugatuzi umesahaulika hivyo basi kuanza kufifia tangu alipoondoka ofisi ya mwenyekiti wa baraza la magavana (CoG).

Akihutubia wanahabari nyumbani kwake Chepalungu, Bw Rutto alisema utekelezaji wa sheria zilizonuiwa kutia nguvu ugatuzi umekwama.

“Hakuna hatua zilizopigwa katika ugatuzi tangu nilipoacha ofisi ya mwenyekiti wa baraza la magava, ajenda nyingi ambazo nilikuwa nikipigania zilikwama,” alisema.

Gavana huyo wa kwanza wa Bomet alisema alipokuwa mwenyekiti wa baraza hilo, alikuwa akishinikiza bodi za huduma za kaunti, zinazoajiri wafanyakazi wa kaunti, ziunganishwe na bodi ya huduma ya umma ya Kenya.

Alisema kuunganishwa na bodi hiyo kutaiwezesha kutekeleza majukumu yake kama tume ya huduma ya umma ambayo inaajiri wafanyakazi wa serikali ya kitaifa.

“Lengo lilikuwa ni bodi za huduma za kaunti ziunganishwe na kuhudumu kama bodi ya huduma ya umma ya Kenya. Hii ingeruhusu wafanyakazi wa kaunti kuhamishwa kutoka kaunti moja hadi nyingine,” alisema.

 

You can share this post!

Kesi ya vyeti feki yazidi kumwandama Samboja

Mutua na Lilian wafunikia kiini cha kutengana