• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Safari ya kisiasa ya Harrison Kombe ambaye mahakama imefuta ushindi wake

Safari ya kisiasa ya Harrison Kombe ambaye mahakama imefuta ushindi wake

NA ALEX KALAMA

HARRISON Kombe ambaye alichaguliwa mbunge wa Magarini kwa mara ya kwanza mwaka 2002 kupitia chama cha Shirikisho, alihudumu kutoka mwaka huo kisha baadaye mahakama ilibatilisha ushindi wake na ilipofika Julai 2007 kuliandaliwa uchaguzi mdogo ambapo alihifadhi kiti chake.

Kwenye uchaguzi mkuu wa Desemba 2007 Kombe alishindwa na Amason Kingi aliyewania kwa tiketi ya ODM.

Mwaka 2013 Kombe alichaguliwa tena kuwa mbunge wa Magarini kupitia chama cha URP ambapo alihudumu kutoka mwaka huo hadi mwaka wa 2017. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 Kombe akiwa URP alishindwa kuhifadhi tena kiti chake kwani alishindwa na Michael Kingi wa chama cha ODM. Wakati huo URP kilikuwa kikiongozwa na rais wa sasa wa Kenya Dkt William Ruto.

Katika uchaguzi mkuu uliopita na ambao ulifanyika Agosti 9, 2022, Kombe wa chama cha ODM alitangazwa mshindi na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ila leo Ijumaa, Machi 3, 2023 Mahakama Kuu ya Malindi imetupilia mbali ushindi wake.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Ucheleweshaji wa malipo ya wakandarasi ukomeshwe

WANDERI KAMAU: Wito kwa Rais William Ruto; waondoe mawaziri...

T L