• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 10:48 AM
Sasa koma kulaumu mahakama, Odinga afokewa na viongozi wa Bonde la Ufa

Sasa koma kulaumu mahakama, Odinga afokewa na viongozi wa Bonde la Ufa

VITALIS KIMUTAI na DAVID MUCHUI

KIONGOZI wa Azimio la Umoja-One Kenya, Bw Raila Odinga ametakiwa akome kushambulia Mahakama baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Baadhi ya viongozi kutoka eneo la Kusini mwa Bonde la Ufa walisema Bw Odinga anafaa kukubali uamuzi wa wapigakura kwenye uchaguzi na uamuzi wa Mahakama ya Juu ulioidhinisha ushindi wa Rais William Ruto wa chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Gavana wa Kaunti ya Kericho, Erick Mutai alisema kwamba Bw Odinga anafaa kustaafu kutoka siasa na kumwachia Rais Ruto na muungano wa Kenya Kwanza nafasi ya kuimarisha uchumi wa nchi.

“Uchumi umedorora, nchi inahitaji kuungana na muungano wa Kenya Kwanza umeanza safari ndefu ya kurejeshea Kenya utukufu wake kitaifa, kikanda na kimataifa,” alisema Dkt Mutai.

Wakati huo huo, Baraza la Wazee wa Jamii ya Ameru la Njuri Ncheke limemhimiza Bw Odinga kukubali kushindwa na kutekeleza jukumu lake kama kiongozi wa upinzani.

Viongozi wa baraza hilo walisema kwamba Kenya inaongoza kwa demokrasia kufuatia uchaguzi wa amani na mchakato wa korti.

Mwenyekiti wa baraza hilo Linus Kathera aliambia wanahabari mjini Meru, akiandamana na wanachama wengine, kwamba wameamua kumsaidia Rais Ruto kushughulikia matatizo ya kiuchumi ya nchi.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Tacos zenye nyama ya kuku iliyookwa

Ziara ya Ruto ng’ambo yazua hisia mseto nchini

T L