• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Seneta wa Kisumu akohoa akiitisha ushahidi wa kutimuliwa chamani

Seneta wa Kisumu akohoa akiitisha ushahidi wa kutimuliwa chamani

NA RICHARD MUNGUTI

KATIKA kile kinachoonekana kama maandalizi ya vita vikali vya kisheria kortini, Seneta wa Kisumu Prof Tom Ojienda ameitisha ushahidi wa maamuzi ya kumtimua chamani kutoka kwa makao makuu ya chama cha Orange Democratic Movement (ODM).

Prof Ojienda ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwakilisha Kaunti ya Kisumu katika bunge la Seneti ameanza kuleta pamoja zana zake za kisheria kukabili ODM mahakamani.

Prof Ojienda amesema uamuzi huo wa kumtimua chamani uko na madhara makubwa katika maisha yake kama mwanasiasa.

“Licha ya kuona matangazo ya kutimuliwa kwangu katika vyombo vya habari, bado ODM haijawasiliana nami,” asema Prof Ojienda katika waraka aliopelekea makao makuu ya ODM katika jumba la Chungwa House.

Prof Ojienda amehoji hatua hiyo ya kumtimua chamani.

Endapo uamuzi huo utaidhinishwa na mahakama yoyote, basi maisha ya kisiasa ya wakili huyo mwenye tajriba ya juu yatayoyoma.

Akieleza kutorodhika kwake, Prof Ojienda ameomba apewe taarifa za majadiliano ya kamati kuu na ile ya nidhamu ya ODM ili aamue hatua atakayochukua ya kisheria.

Katika waraka uliopelekwa kwa ODM na kampuni ya mawakili ya Prof Tom Ojienda & Associates mnamo Septemba 7, 2023, seneta huyo amesema ameathiriwa na uamuzi huo wa kumtimua chamani kwa sababu ya kushirikiana na muungamo tawala wa Kenya Kwanza.

Kampuni hiyo ya mawakili imesema chama cha ODM hakijawasiliana na Prof Ojienda,ile amesoma katika vyombo vya habari ametimuliwa.

“Tunaomba taarifa za majadiliano ya kamati ya nidhamu ya ODM kabla ya kufikia uamuzi wa kumtimua chamani Prof Ojienda,” makao makuu ya ODM yameelezwa na kampuni hiyo ya mawakili.

Barua hiyo imenakiliwa wakili Nelson Havi.

Mbali na Prof Ojienda wengine waliotimuliwa ni pamoja na Mbunge wa Lang’ata Felix Odiwuor almaarufu Jalang’o, Paul Abuor (Rongo), Elisha Odhiambo (Gem) na Caroli Omondi (Suba).

  • Tags

You can share this post!

Wanamapinduzi Gabon wamwachilia Bongo ‘anayeugua’

Watoaji elimu ya maabara ya tiba watozwa faini ya Sh800,000...

T L