• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Sonko aachwa nje na IEBC

Sonko aachwa nje na IEBC

NA CHARLES WASONGA

GAVANA wa zamani wa Nairobi Mike Sonko amepata pigo baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kukosa kuchapisha jina lake kwenye gazeti rasmi la serikali kama mgombeaji wa ugavana, Mombasa.

Hii ni kutokana na kesi ambayo aliwasilisha katika Mahakama Kuu ya Mombasa kupinga hatua ya kamati ya tume hiyo kutatua mizozo kumzima kuwania.

Katika kesi hiyo, Bw Sonko anaitaka mahakama kuizuia IEBC kuchapisha majina ya wagombeaji ugavana Mombasa hadi kesi yake itakapoamuliwa.

Mwanasiasa huyo pia anaitaka mahakama kuamuru IEBC kumwidhinisha kama mgombea ugavana wa Mombasa kwa kupokea vyeti vyake vya shahada ya digrii.

Kesi hiyo imeratibiwa kuamuliwa mnamo Ijumaa, Julai 15, 2022.

IEBC pia imekosa kuchapisha jina la Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo kama mgombeaji wake wa ugavana wa Mombasa kuchukua pahala pa Bw Sonko.

Hii ni licha ya kwamba chama cha Wiper kiliwasilisha jina la Bw Mbogo kwa IEBC mnamo Julai 9.

Mwingine ambaye jina lake halijachapishwa katika toleo hilo la gazeti rasmi na Bw Karungo Wa Thangwa anayewania useneta wa Kiambu kwa tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Hii ni licha ya kwamba mnamo Alhamisi wiki jana, Mahakama Kuu ilibatilisha hatua ya IEBC kumzima mwanasiasa huyo kugombea kiti hicho kwa misingi kuwa alitumuliwa afisini kwa tuhuma za ufisadi.

Katika uamuzi wake, Jaji Rachel Ng’etich alikubaliana na utetezi wa Wa Thang’wa kwa hakuna ushahidi kwamba alivuliwa wadhifa wa uwaziri katika serikali ya kaunti ya Kiambu kutokana na uovu huo.

Hata hivyo, seneta wa Nairobi Johnson Sakaja na mwenzake wa Kakamega Cleophas Malala wameidhinishwa kuwa wagombeaji ugavana Nairobi na Kakamega, mtawalia.

Hii ni licha ya utata unaogubika uhalali wa vyeti vyao vya shahada za digrii, ambao angali kuamuliwa mahakamani.

  • Tags

You can share this post!

Simanzi kijana akiuawa na genge

Euro 2022: Vipusa wa Ureno watoka nyuma na kulazimishia...

T L