• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Tutaheshimu uamuzi wa mahakama ya rufaa kuhusu BBI – Raila

Tutaheshimu uamuzi wa mahakama ya rufaa kuhusu BBI – Raila

Na SAMMY WAWERU

KIONGOZI wa ODM, Bw Raila Odinga ametangaza kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama ya rufaa kuhusu hatma ya Ripoti ya Mswada wa Maridhiano (BBI).

Makama kuu iliharamisha mswada huo wa 2020 unaopendekeza marekebisho ya Katiba, baada ya baadhi ya wanaharakati na mashirika kuupinga.

Waanzilishi wa BBI, Bw Odinga na Rais Uhuru Kenyatta, walikata rufaa, uamuzi ukitarajiwa kutolewa Agosti 2021.

Bw Odinga kwa mara ya kwanza ametangaza ataheshimu maamuzi yatakayotolea.

“Nina uhakika majaji watatekeleza haki, ni wasomi na wanajua haki. Hata hivyo, uamuzi utakaotolewa tutauheshimu,” akasema.

Akifufua makovu ya ushindi wake kiti cha urais 2007, 2013 na 2017, kwa kile alitaja kama “nilitolewa nyama mdomoni”, Bw Raila alisema ametoka mbali.

Alisisitiza kwamba yeye ni mtetezi mkuu wa demokrasiaKenya na anaiheshimu, hivyo basi hatakuwa na budi kukubali maamuzi ya mahakama ya rufaa.

“Sisi ni watu wanoamini demokrasia. Tumetoka mbali, tumetoka mashimoni. Hali tuliyopo nayo sasa ya uhuru wa kuongea tuliitetea.

“Ikiwa mahakama itaamua dhidi yetu (akimaanisha kutia saini muhuri uamuzi wa mahakama kuu), tutaheshimu ,” akasisitiza.

You can share this post!

‘Corona imenisukuma kwa kona’

Sitajiuzulu kama Spika, Muturi asema