• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 PM
Uhuru akana kuwa anapanga kuua Dkt Ruto na wandani wake katika Kenya Kwanza

Uhuru akana kuwa anapanga kuua Dkt Ruto na wandani wake katika Kenya Kwanza

NA CHARLES WASONGA

MALUMBANO kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuhusu siasa za urithi yaliendelea kushuhudiwa Jumapili, Agosti 31, 2022.

Hii ni baada ya Rais Kenyatta kukana kupanga kumuua Dkt Ruto na wandani wake wa karibu, walivyodai Dkt Ruto na mgombea mwenza wake wa urais Rigathi Gachagua juzi.

Akiongea alipoongoza hafla ya ufunguzi rasmi wa barabara ya moja kwa moja, Nairobi Expressway, Rais Kenyatta alieleza kuwa kwa miaka mitatu iliyopita Dkt Ruto na wandani wake wamekuwa wakimtusi huku akikimya tu.

Alisema kuwa wakati mwafaka kwake kuwachukulia “hatua yoyote ile” ilikuwa wakati huo, na wala sio sasa ambapo anakamilisha muhula wake wa pili na wa mwisho afisini.

“Hiyo sio ajenda yangu wakati huu,” Rais Kenyatta akasema.

“Haina haja wewe kuwaambia watu kwamba ninataka kukuua. Si umenitusi kwa miaka mitatu na hakuna mtu amekugusa. Si nimekuwa serikalini kwa miaka mitatu na nilikuwa na mamlaka yote?” Rais Kenyatta akauliza.

“Je, wakati huu ambapo ninakaribia kupokeza mtu mwingine hatamu za uongozi, ndipo unahisi kwamba ninakuandama?” akauliza tena.

Rais Kenyatta alisisitiza kuwa hamna haja kwa Dkt Ruto na wenzake kumtusi kwa sababu kile amekuwa akifanya ni kuwaonya Wakenya dhidi ya kukubali awadanganye hadharani.

“Usiendelee kuwadanganya watu na ninapojibu uwongo wako usiwaambie watu kwamba ninataka kukuua. Wewe uza ajenda yako na porojo nyinginezo na uachane nami. Nitaendelea na kazi yangu hadi nikamilishe. Wewe tafuta kura kutoka kwa wananchi, wakikuchagua sawa, wakikosa kukuchagua basi tutaenda nyumbani pamoja,” Rais Kenyatta akaeleza.

Akiongea katika msururu wa kampeni mjini Kapsabet, Kaunti ya Nandi na maeneo ya karibu, Dkt Ruto alisema haogopi kupambana na Rais Kenyatta na “mradi” wake, Raila Odinga, debeni.

“Mradi hautaua watoto wangu, niko tayari kukabiliana nawe katika uchaguzi huu, ukiwa pamoja na mradi wako, huyo mzee wa kitendawili,” Dkt Ruto akasema mjini Kapsabet.

“Bw Rais, umekuwa chanzo cha vitisho nchini Kenya. Koma kutisha Wakenya. Kazi yako ni kuhakikisha kuwa Wakenya wote wako salama. Koma kutuambia kwamba tutajua wewe ni Rais,” Naibu Rais akafoka huku akionekana mwenye hasira.

Dkt Ruto alisema kuwa vitisho dhidi yake havitamzuia kuendelea na juhudi zake za kusaka kura za urais.

“Koma kunikabili rafiki yangu, tafadhali endelea kumfanyia kampeni mgombeaji chaguo lako. Bw Rais, tafadhali koma kuongea juu yangu, ongoea kuhusu mtu wako. Tuambia ajenda ya mzee wa kitendawili na uachane na William Ruto kabisa,” Dkt Ruto akasema.

Siku moja baadaye, Bw Gachagua pia alifuata nyayo za Dkt Ruto kwa kumkaripia vikali Rais Kenyatta kwa kile alichadai ni kutishia maisha yake.

Akiendesha kampeni katika kaunti ya Nyeri, Gachagua ambaye ni Mbunge wa Mathira aliongeza kuwa maisha ya wenzake; Moses Kuria, Kimani Ichang’wa na Ndindo Nyoro pia yamo hatarini.

Bw Kuria ni mbunge wa Gatundu Kusini, Ichungwa ni mbunge wa Kikuyu ilhali Bw Nyoro ni Mbunge wa Kiharu; wote ni wandani na watetezi s

  • Tags

You can share this post!

Mwenyekiti wa Bodi ya NMG ahimiza amani

Mshukiwa wa ujambazi akamatwa akiwa na sare za wanajeshi,...

T L