• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Wa Iria azua rabsha Bomas akitaka kibali cha kuwania urais

Wa Iria azua rabsha Bomas akitaka kibali cha kuwania urais

NA LEONARD ONYANGO

GAVANA wa Murang’a Mwangi Wa Iria alizua sarakasi katika ukumbi wa Bomas, Nairobi, akipinga kuachwa nje ya kinyang’anyiro cha urais.

Bw Wa Iria alisababisha kizaazaa huku msanii wa ucheshi Walter Mong’are Nyambane akiwa mwaniaji wa kwanza wa urais kuidhinishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Bw Iria alifunga malango ya kuingia na kutoka Bomas kwa magari yaliyokuwa na picha na rangi za chama chake cha Usawa, huku akicheza muziki wa juu na kuapa kutumia kila mbinu kuhakikisha atakuwa debeni Agosti 9.

Sarakasi hizo za Gavana wa Murang’a zilitatiza shughuli za IEBC kwa muda hadi maafisa wa usalama wakatumwa Bomas kudumisha Amani.

Gavana huyo alitishia kubadilisha chama chake cha Usawa kuwa vuguvugu la kupinga serikali iwapo hataidhinishwa kuwania urais.

Bw Wa Iria alishikilia kuwa alipeleka idadi ya saini zinazohitajika.

Jana Jumatatu, Profesa George Wajackoyah wa chama cha Roots alikosa kuidhinishwa kwa kukosa saini za kutosha za watu wanaomuunga mkono.

Kulingana na Bw Chebukati, Prof Wajackoyah alikuwa na saini za wanaomuunga mkono kutoka kaunti 17 badala ya 24.

Wengine waliotemwa ni Patrick King’ori na Justus Juma.

Leo Jumanne wanaotarajiwa kufika mbele ya Bw Chebukati ni Bi Dorothy Kemunto Nyangori, Bw James Kamau na Bw Gibson Ngaruiya Nganga.

  • Tags

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Mradi wa Arror umekwama licha ya ripoti...

Wanafunzi wenye historia ya utukutu kuzimwa kuajiriwa

T L