• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Wamaasai waonya Tangatanga dhidi ya kujaribu kupenya Narok

Wamaasai waonya Tangatanga dhidi ya kujaribu kupenya Narok

Na GEORGE SAYAGIE

VIONGOZI kutoka jamii ya Wamaasai wameonya kundi la wanasiasa wa kundi la ‘Tangatanga’ dhidi ya kujaribu kujipenyeza katika Kaunti ya Narok wakisema eneo hilo ni ngome ya handisheki.

Tangatanga inamuunga Naibu Rais William Ruto kuwania urais mwaka ujao.

Onyo hilo linajiri huku ubabe kwa kisiasa kati ya kundi hilo na wanasiasa wanaounga mkono handisheki kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM, Raila Odinga, ukiendelea kushika kasi.

Jumanne, mbunge Moitalel Kenta (Narok Kaskazini), Bw Kelena Nchoe wa Baraza la Wazee wa Wamaasai (MCC) na diwani maalum Christine Lemein walipuuzilia mbali madai ya kundi hilo kwamba, kaunti hiyo ni ngome ya kisiasa ya Dkt Ruto.

Badala yake, walisisitiza kuwa kaunti hiyo inaunga mkono handisheki na hawawezi kuruhusu siasa za migawanyiko kuendeshwa humo. “Kama baraza la wazee, tunajua upande tutakaowapeleka watu wetu. Tangatanga wanapaswa kukaa mbali,” akasema Bw Nchoe.

 

You can share this post!

Safari ya mwisho ya Ayimba yaanza na misa ya wafu South B

Rais wa Ufaransa azabwa kofi na mkazi