• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Wawaniaji wa urais washawishi majopo ya IEBC yawarudishe debeni

Wawaniaji wa urais washawishi majopo ya IEBC yawarudishe debeni

NA RICHARD MUNGUTI

WAWANIAJI kiti cha urais waliokataliwa Alhamisi walifanya kila juhudi wakati wa kipindi cha lala salama kubatilisha uamuzi wa kuwatupa nje.

Wakiongozwa na mwaniaji wa urais kwa tikiti ya chama cha Safina Jimi Wanjigi, Dkt Ekuro Aukot wa Thirdway Alliance anayeomba uidhinshwaji wa Raila Odinga ubatilishwe kwa vile muungano wa Azimio hauwezi kumteua kwa vile sio chama cha kisiasa na wawaniaji wengine, waliomba majopo ya IEBC yaamuru waidhinishwe kuwania urais.

Lakini Wanjigi alipata pigo kubwa ombi lake la kutaka mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati afike kortini kuhojiwa kutokana na uamuzi wa kukataa kumwidhinisha lilipotupiliwa mbali.

Jopo linaloongozwa na George Mburugu lilitupilia mbali ombi la Wanjigi kupitia wakili Willis Otieno likisema “halina mamlaka na uwezo kisheria kumwagiza Chekubati afike mbele ya jopo kuhojiwa.”

Bw Mburugu aliamuru Bw Otieno aendelee na kesi ya kupinga uamuzi huo wa Chebukati.

Wanjigi alifurushwa nje ya kinyang’anyiro cha Urais kwa sababu hana Digrii kutoka Chuo kikuu kinachotambulika.

Lakini amejitetea akisema atahitimu na Digrii Novemba 22, 2022.

Aliwasilisha barua kutoka Chuo Kikuu cha Daystar kuthibitisha amekuwa akisomea huko.

Na wakati huo huo jopo hilo liliondoa jina la Chuo hicho cha Daystar katika kesi hiyo likisema “hakikuhusika kwa njia yoyote ile katika harakati za uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.”

Bw Otieno aliomba jopo hilo lisikilize na kuamua malalamishi yote kwa vile kipindi chao cha siku 10 cha kusikiliza na kuamua malalamishi kitamalizika Juni 17, 2022.

“Naomba kamati hii iamue kesi hizi kabla ya Juni 17, 2022 ,” alisema Bw Otieno.

Chebukati pia alisema sababu nyingine ya kumnyima Wanjigi uteuzi ni kwa vile hakuwa ameidhinishwa na wapiga kura 48,000 kutoka kaunti 24.

IEBC pia ilisema wawaniaji wengine wa kiti cha Urais waliowasilisha malalamishi ni pamoja na Dkt Aukot wa chama cha Thirdway Alliance anayeomba Chebukati amlambishe sakafu mwaniaji wa uraisa wa Azimio Raila Odinga kwa madai Azimio sio chama cha kisiasa mbali ni muungano wa vyama vingi.

“Azimio hakiwezi kumateua mwaniaji wa urais kwa vile sio chama cha kisiasa,” anasema Dkt Aukot.

Wengine waliofika mbele ya majopo hayo kujaribu bahati yao ya mwisho ikiwa wanaweza rudishwa katika debe la kura ni pamoja na Walter Mong’are, Reuben Kigame na Ojijo Ogillo Mark Pascal.

Reuben Kagame (mwenye tai nyekundu) aliyenyimwa uidhinishwaji kuwania urais na IEBC. PICHA | RICHARD MUNGUTI

Mong’are alikuwa ameteuliwa lakini uteuzi wake ukaharamishwa kasoro ilipoguduliwa katika cheti chake cha Digrii.

Hata hivyo alipewa muda hadi Ijumaa awasiliane na chuo kikuu cha Kenyatta (KU) aidhinishiwe cheti chake cha Digrii.

Jopo hilo linaloongozwa na wakili Paul Lilan ilifuta jina la chuo kikuu cha Daystar katika kesi hiyo kwa vile hakikuhusika na suala la uteuzi.

Bw Lilan alisema endapo chuo hicho kitahitajika kujibu swali lolote basi afisa wake mkuu Paul Mbuta atajibu.

“Chuo cha Daystar kimeweka afidaviti hapa kortini ikijadili masuala yote kuhusu kesi hii,” alisema Bw Lilan.

Majopo matatu yanayoamua mizozo ya uidhinishwaji wa wawaniaji yatatoa maamuzi yao kabla ya Juni 20,2022.

Miongoni mwa washtakiwa waliopata furaha isiyo na kifani ni pamoja Mbunge wa Dagoretti Kaskazini Simba Arati walamishi wawili waliopinga akiwania Ugavana Kisii kuondoa kesi dhidi yake.

Wapiga kura hao wawili kupitia wakili wao Peter Wanyama walieleza Jopo kwamba “Arati amehitimu kwa Digirii ya Uzamili na Digirii ya kwanza kutoka chuo kikuu cha cha kiufundi cha Jaramogi Odinga Oginga.”

Bw Wanyama aliikabidhi jopo hilo digirii hizo mbili na kuomba “kesi dhidi ya Arati itamatishwe.”

Bw Arati aliwakilishwa na wakili Alfred Nyandieka aliyesema mwaniaji kiti huyo cha ugavana aliharibiwa sifa na kushushiwa hadhi kwa madai hajahitimu kwa digirii.

Jopo hilo liliamuru walalamishi waliomharibia sifa katika vyombo vya habari warudi mle wakatangaze Arati amehitimu na yuko na digrii ya uzamili.

Wanyama alilikabidhi jopo hilo digrii zote za Arati na kuomba kesi itamatishwe.

Na wakati huo aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko aliomba jopo linaloongozwa Bw Wambua Kilonzo liamuru IEBC imwidhinishe kwa vile amehitimu.

  • Tags

You can share this post!

UJASIRIAMALI: Watengeneza miswaki kwa mianzi kulinda...

Bei za juu za bidhaa zagonga raia vibaya

T L