• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 9:49 AM
Zogo wafuasi wa UDA na ANC wakilumbana

Zogo wafuasi wa UDA na ANC wakilumbana

NA SHABAN MAKOKHA

UHASAMA kati ya vyama vya UDA na ANC katika kaunti ya Kakamega unatishia umoja wa muungano wa Kenya Kwanza huku wanachama wa vyama hivyo viwili waking’ang’ana kuvivumisha kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Mzozo kati ya vyama hivyo umevuruga mipango ya kufanya mikutano ya pamoja ya kampeni.

Maeneo yaliyoathiriwa mno na zogo hilo ni Butere, Mumias Mashariki, Matungu, Mumias Magharibi na Sabatia katika kaunti ya Vihiga ambako muungano wa Kenya Kwanza una wawaniaji wa ubunge kwa tikiti za UDA na ANC.

Katika eneo la Butere, Michael Keya (UDA) anashindana na Habil Nanjendo (ANC), na huko Matungu, Alex Lanya (ANC) anamenyana na Paul Posho (UDA).

Katika eneo la Mumias Magharibi, Rashid Echesa (UDA) anashindana na Jackline Okanya (ANC) huku kule Mumias Mashariki David Wamatsi (ANC) akikabiliana na Benjamin Mapwoni (UDA).

Seneta Cleophas Malala, ambaye ni mgombea ugavana wa Kenya Kwanza kaunti ya Kakamega anakabiliana na mwaniaji wa kiti cha useneta Boni Khalwale na mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali.

Bw Malala anagombea kwa tikiti ya chama cha ANC kinachoongozwa na Musalia Mudavadi naye Bw Khalwale ni mwanachama wa UDA.

Bw Washiali aliyejiondoa kutoka uchaguzi ni mwanachama wa UDA na anaongoza kampeni za Naibu Rais katika eneo la Magharibi.

Bw Khalwale na Bw Washiali wamechagua kupigia debe wawaniaji wa UDA dhidi ya wale wengine katika muungano wa Kenya Kwanza.

Kizaazaa kilitokea katika shule ya sekondari ya Isongo Jumamosi na vita vikazuka kati ya wafuasi wa Bw Wamatsi na Mapwoni baada ya Bw Khalwale na Washiali kupigia debe mwaniaji wao– Bw Mapwoni lakini wakakataza Bw Malala kuendesha kampeni za mwaniaji wa ANC, Bw Wamatsi.

Bw Washiali, aliyemwidhinisha Mapwoni kuwa mgombeaji wa UDA wa kiti cha ubunge alisema kuwa mradi mwaniaji wao ametimiza mahitaji yote, watamuunga mkono hadi kwenye debe.

Bw Malala alisema kwamba iwapo muungano wao utaanza kutenga maeneo huenda wakakosa kushinda.

“Kuna haja yetu katika Kenya Kwanza kufanya kazi kama kundi moja. Tukiendelea hivi, tutapoteza kaunti hii kwa Azimio,” alisema Malala.

  • Tags

You can share this post!

Wataalamu waunga Muthama ugavana

MAPISHI KIKWETU: Jinsi unavyoweza kuandaa sandiwichi...

T L