• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Njuki adai hatua ya Uhuru kuunga Raila imechemsha nchi

Njuki adai hatua ya Uhuru kuunga Raila imechemsha nchi

NA ALEX NJERU

GAVANA wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki amedai kuwa uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta kumuunga mkono mwaniaji wa urais wa muungano wa Azimio umechangia kupandisha joto la kisiasa nchini.

Akiongea katika Kanisa Katoliki la St Joseph’s eneobunge la Chuka/Igambang’ombe mnamo Jumatatu, Bw Njuki alisema hatua ya Rais Kenyatta kumuidhinisha Bw Raila Odinga, imewalazimu watumishi wote wa umma kumuunga mkono.

Hata hivyo, gavana huyo alisema mgombea urais wa Kenya Kwanza William Ruto na wafuasi wote wa muungano huo wanatarajia kuwa Bw Odinga akishindwa, Rais Kenyatta atakubali matokeo hayo.

“Taharuki imepanda uchaguzi mkuu unapokaribia kwa sababu ameamua yule ambaye atakuwa mrithi wake. Wananchi wako na wasiwasi ikiwa Bw Kenyatta atampokeza mshindi mamlaka akishindwa (Raila akishindwa),” akasema Bw Njuki.

Gavana huyo alitoa wito kwa viongozi wa kidini kuombea amani idumu kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu ujao.

“Hii ndio njia ya kipekee ya kuepuka ghasia sawa na zile zilizoshuhudiwa nchini,” Bw Njuki akasema.

  • Tags

You can share this post!

Wakenya kula ugali nafuu kwa mwezi 1

TUSIJE TUKASAHAU: Hadaa za viwanja, kulikoni?

T L