• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Hadaa za viwanja, kulikoni?

TUSIJE TUKASAHAU: Hadaa za viwanja, kulikoni?

WALIPOZINDUA manifesto yao kuelekea uchaguzi mkuu wa 2013, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliahidi kujenga viwanja tisa vya michezo sehemu mbalimbali nchini.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa manifesto hiyo katika uwanja wa michezo wa Kasarani, Nairobi, Dkt Ruto alisema kuwa miradi hiyo ingekamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya wao kuingia mamlakani.

“Ndani ya miezi sita uwanja wa michezo mjini Wote utakuwa umekamilika. Ndani ya miezi mitatu uwanja wa michezo wa Chuka utakuwa umekamilika. Ndani ya miezi mitatu uwanja wa michezo wa Moyale utakuwa umekamilika. Uwanja wa michezo wa Kamariny katika Kaunti ya Pokot Magharibi, ambao ni wa kihistoria pia utakuwa umekamilika,” akasema Dkt Ruto.

Lakini miaka 10 baadaye ripoti za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali zinaonyesha kuwa ujenzi wa viwanja hivyo haujakamilika.

Dkt Ruto atakapotua mjini Wote leo Jumanne kuendesha kampeni ya kusaka kura za uraia, asije akasahau kuelezea wakazi sababu zilizochangia kukwama kwa mradi huo.

  • Tags

You can share this post!

Njuki adai hatua ya Uhuru kuunga Raila imechemsha nchi

Umaarufu wa Kidero tishio kwa ubabe wa ODM Nyanza

T L