• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:50 AM
Pwani yaongoza kwa idadi ya magenge nchini

Pwani yaongoza kwa idadi ya magenge nchini

 MOHAMED AHMED na LEONARD ONYANGO

UKANDA wa Pwani unatambulika kuwa miongoni mwa maeneo yenye idadi kubwa ya magenge hatari.

Kati ya makundi ya awali ni Kayabombo na Mombasa Republican Council (MRC), ambalo baadaye mahakama lililitaja kuwa si haramu.

Katika siku za hivi punde, wakuu wa usalama Pwani wamekumbana na mwamko mpya wa makundi hatari, ambapo baadhi hutumia hata bunduki katika mashambulio.

Magenge mengine ni ya vijana wenye umri mdogo ambao wamekuwa wakivamia wakazi.

Miongoni mwa magenge hayo ni, Wakali Kwanza, Wakali Wao, Military, Gaza, Buffalo, Home Boys, Chafu za Down na Gater Family,

Mengine ni Kapenguria six, Young Thugs, Spanish Spatter, Gaza, Mawaiyo, Crazy Boys, Born to Kill, Vietnam, Akili za usiku, 64 Gang, Memory Gang, Watalia Gang, Temeke, KaduAsili Networks kati ya mengineyo mengi.

Mwezi uliopita, watu wawili walishambuliwa na genge la watu waliokuwa wamebeba mapanga katika eneo la Soko Mjinga, Kisauni Mombasa.

Mapema mwezi jana, polisi walimuua mshukiwa kwa kumpiga risasi, ambaye alikuwa mwanachama wa genge la wahalifu ambao wamekuwa wakihangaisha wakazi wa Kisauni.

Mshukiwa huyo alidaiwa kusimamisha matatu katika barabara ya Bamburi-CBF na kuwaibia abiria saa 12 asubuhi.

Washukiwa hao walimkata mwanafunzi wa kike wa Chuo cha Technical kabla ya kumwibia.

Mwaka jana, genge la wahalifu waliokuwa wamevalia sare za polisi lilishambulia wakazi wa kijiji cha Kadza Ndani, eneobunge la Kisauni katika Kaunti ya Mombasa na kuua mtu mmoja huku wengi wakijeruhiwa.

Idara ya Upepelezi wa Jinai (DCI) mwezi uliopita ilisema kuwa inawachunguza madiwani wawili wanaodaiwa kufadhili magenge ya ‘Wakali Kwanza’ na ‘Wajukuu wa Bibi’ katika maeneo ya Kisauni na Likoni.

You can share this post!

Maaskofu wasema mkutano wa Ruto lazima ufanyike

Wachoshwa na genge la Sangwenya, wamtaka Matiang’i...

adminleo