• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:25 PM
Madeni yatisha kuhujumu ujenzi wa barabara kuunganisha miji

Madeni yatisha kuhujumu ujenzi wa barabara kuunganisha miji

Na BERNARDINE MUTANU

Huenda ujenzi wa barabara kubwa inayounganisha miji mikuu nchini moja kwa moja kwa gharama ya Sh350 bilioni ukakwama kwa muda.

Hii ni kutokana na hofu ya viongozi kwamba huenda Kenya ikashindwa kuhimili uzito wa madeni mengi.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa kampuni iliyopewa kandarasi ya kujenga barabara hiyo. Mikopo mingi ya ujenzi wa barabara nchini inachukuliwa kutoka kwa serikali ya Uchina.

Jinsi ilivyo, huenda deni la serikali likaongezeka hadi asilimia 58 ya mapato yote ya taifa kufikia mwishoni mwa Juni mwaka huu, kutoka asilimia 40.6 mwaka wa kifedha wa 2011/12 kulingana na makadirio ya Benki ya Dunia.

Ujenzi wa barabara ya kilomita 473 kati ya Nairobi na Mombasa unaendeshwa na kampuni ya San Francisco, Bechtel Group, ambayo inafanya hivyo kupitia kwa mkopo iliyokubaliana na serikali.

Lakini kulingana na Mamlaka ya Barabara Kuu(KeNHA) haina habari zozote kuhusu kucheleweshwa kwa mradi huo, alisema Charles Njogu, afisa wa mahusiano ya umma wa KeNHA.

Hata hivyo, alisema lazima mradi huo ukaguliwe na viongozi hasa kutokana na ukubwa wake.

You can share this post!

Rift Valley Railways yawekewa vikwazo na IMF sababu ya...

Azma ya Gladys Wanga kugeuza chama kuwa benki

adminleo