• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Starlets waanza kunoa kucha za kuiumiza Equatorial Guinea

Starlets waanza kunoa kucha za kuiumiza Equatorial Guinea

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya almaarufu Harambee Starlets imeripoti kambini Mei 23, 2018 kujiandaa kupepetana na Equatorial Guinea katika mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Afrika nchini Ghana baadaye mwaka huu.

Warembo wa kocha David Ouma watafanyia mazoezi yao katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos kuanzia Alhamisi jioni.

Starlets wataalika mabingwa hawa wa zamani wa Afrika kwa mechi ya mkondo wa kwanza hapo Juni 6 kabla ya kuzuru taifa hilo linalopatikana Magharibi mwa Afrika kwa mchuano wa marudiano mnamo Juni 9.

Ouma na warembo wake walishiriki makala yaliyopita nchini Cameroon na wana hamu kubwa ya kuwa nchini Ghana. Hata hivyo, Equatorial Guinea ni timu kali na watalazimika kufanya kazi ya ziada kupata tiketi.

Starlets walitolewa kijasho katika raundi ya kwanza pale waliponyuka Uganda 1-0 humu nchini kabla ya kutoka sare tasa katika mechi ya marudiano jijini Kampala.

Kikosi cha Starlets:

Makipa – Poline Atieno (Makolanders), Annette Kundu (Eldoret Falcons), Maureen Shimuli (Wadadia), Lilian Awuor (Vihiga Queens);

Mabeki – Wendy Achieng (Spedag), Dorcas Sikobe (Oserian Ladies), Doris Anyango (Spedag), Elizabeth Ambogo (Spedag), Phelistus Kadari (Vihiga Queens), Lilian Adera (Vihiga Queens), Vivian Nasaka (Vihiga Queens), Anita Adongo (Oserian Ladies);

Viungo – Cheris Avilia (Spedag), Ruth Ingosi (Eldoret Falcons), Sheryl Angachi (Gaspo Youth), Corazon Aquino (Vihiga Queens), Faith Kwamboka (Thika Queens), Caroline Anyango (Spedag);

Washambuliaji – Mwanahalima Adam (Thika Queens), Mercy Achieng (Thika Queens), Neddy Atieno (Makolanders), Esse Akida (Spedag), Janet Bundi (Eldoret Falcons), Teresa Engesha (Vihiga Queens), Cynthia Shilwatso (Vihiga Queens), Mary Kinuthia (Gaspo Youth).

You can share this post!

KRA na NBK kuwapa vijana mafunzo ya ushuru na uwekezaji

#JudiciaryForTheRich: Mahakama yashambuliwa kwa kuwanyima...

adminleo