• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Linturi alaumu Rais kwa kupuuza kilio cha Wakenya

Linturi alaumu Rais kwa kupuuza kilio cha Wakenya

Na GITONGA MARETE

SENETA wa Meru Mithika Linturi amemlaumu Rais Uhuru Kenyatta kwa kupuuza matatizo ya Wakenya na kushughulika na masuala ambayo hayana umuhimu kwa nchi.

Bw Linturi alimuomba kiongozi wa nchi kusikiliza kilio cha Wakenya akisema wanapitia hali ngumu kutokana na athari za virusi vya corona kwa uchumi.

Kulingana na seneta huyo, serikali inafaa kubuni mbinu za kulinda Wakenya kutokana na athari hizo.Alisema kwamba afueni ambayo serikali ilikuwa imepatia Wakenya kwa kupunguza viwango vya kodi inafaa kuendelea kwa sababu janga hilo bado haliko karibu kuangamizwa.

“Serikali haijawapatia Wakenya mwelekeo kuhusu jinsi itakavyowalinda dhidi ya janga la corona ilhali tunashughulika na kura ya maamuzi na kutenga Sh94 milioni za kukagua saini. Hii ni licha ya kuwa wahudumu wa afya wanagoma kwa kutolipwa mishahara kwa miezi kadhaa.

Viongozi wa nchi hii wanafaa kuzinduka,” alisema Bw Linturi alipohudhuria mazishi ya dada wa Gavana wa Meru, Bw Kiraitu Murungu, Bi Jane Riara, 64. Bw Linturi alisema inashangaza Bima ya Afya (NHIF) haiwezi kuwafaa wanaougua corona.

“Tunaambia watu nini kweli? Kwamba kuna janga na tunafaa kuwasahau na kushughulika na vitu kama BBI? Hapana, nchi hii imepoteza mwelekeo.”

You can share this post!

Arteta aahidi mashabiki wa Arsenal makuu

Mamia Mlima Kenya waombea corona itokomee