Wanachama wa chama tawala cha Zimbabwe wadungwa chanjo ya COVID-19 ya Sinopharm

Na MASHIRIKA

MAAFISA wa chama tawala cha Zimbabwe ZANU-PF na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho leo wamedungwa chanjo ya Covid-19 ya Sinopharm, wakati nchi inaharakisha kuhakikisha kuwa watu wengi zaidi wanadungwa chanjo hiyo.

Kupitia mtandao wa Twitter, chama hicho kiliandika kuwa, Katibu Tawala wa Taifa Obert Mpofu ameongoza mpango wa kutoa chanjo, ambapo wenzake wa Kamati ya Sera wameshashiriki na kuonyesha imani yao kwa chanjo ya China.

Kwa mujibu wa Katibu wa Afya na Wazee wa chama hicho David Parirenyatwa, ZANU-PF kimewataka wafanyakazi wake wote kudungwa chanjo.

CRI

Habari zinazohusiana na hii