• Nairobi
  • Last Updated May 29th, 2023 9:37 PM
Aibu tupu mke wa mwanasiasa kukataa kuandalia wafuasi chai

Aibu tupu mke wa mwanasiasa kukataa kuandalia wafuasi chai

NA NICHOLAS CHERUIYOT

ABOSI, SOTIK

MWANASIASA limbukeni kutoka eneo hili alipata aibu ya mwaka mkewe alipohepa bila kuandalia chai wafuasi wa jamaa huyo waliofika kwake kutangaza kuwa watamuunga mkono.

Inaarifiwa kuwa makalameni na warembo waliodai ni wafuasi wa mheshimiwa walifika ghafla kwa na kuimba wimbo wa kumsifu mwenyeji wao.

Jamaa aliagiza mkewe aingie jikoni atayarishe chai na mandazi huku akielekeza wageni waketi awauzie sera zake.

“Baada ya kusuburi kwa muda, jamaa aliekea jikoni ambapo hakukuwa na dalili ya chai. Mkewe alimtumia arafa kumwarifu alienda kufanya shughuli zake. Wafuasi waliondoka wakiwa na njaa wakilia mke wa mheshimiwa ni mchoyo,” mdokezi aliarifu.

Mkewe alifahamisha marafiki alijua tu hao walikuwa walofa waliotaka kufyonza mumewe.

You can share this post!

Chepng’etich arejea Japan kwa kishindo Nagoya Marathon

Wetang’ula sasa ataka Raila akamatwe

T L