• Nairobi
  • Last Updated May 29th, 2023 9:37 PM
Waya ya stima yakatiza uraibu wa kozimeni aliyetesa wenyeji

Waya ya stima yakatiza uraibu wa kozimeni aliyetesa wenyeji

DIMBWINI LIKONI

Na DOMINIC MAGARA

TABIA YA MLOFA mmoja kuchungulia madirisha ya watu wakiwa wamelala, imefikia kikomo pale alipogusa waya za stima na kurushwa mbali.

Wakazi wa mtaa huu waliamshwa na kelele usiku wa manane wakidhani walikuwa wamevamiwa na wezi.Kwa mshangao, walimpata kalameni, jirani yao akiwa anagaa gaa kwa maumivu makali na kuomba msaada kupelekwa hospitali. Uchunguzi wa haraka ulibaini kwamba, alirushwa na waya wa stima.

Inadokezwa kwamba, bila kuona aibu wala kusita, alieleza masaibu yake. Alijitambulisha kama mmoja wa makosimeni mtaani, wanaojulikana kwa kuchungulia madirisha ya watu usiku wakiwa wamelala.

Furaha ya kutazama sinema katika nyumba za watu iligeuka kuwa balaa pale alipopata jeraha kubwa na maumivu makali.

You can share this post!

Wakazi mjini Moi’s Bridge sasa wapumua

Nairobi Water Queens balaa katika Handiboli nchini

T L