• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
Zaidi ya vyuo 500 vya udereva hatarini kufungwa

Zaidi ya vyuo 500 vya udereva hatarini kufungwa

Na BRIAN WASUNA

MAMIA ya vyuo vya kutoa mafunzo ya udereva ziko katika hatari ya kufungwa kufuatia hatua ya Mamlaka ya Usalama Barabarani (NTSA) kuzitaka kutuma upya maombi ya leseni.

NTSA imeagiza vyuo zaidi ya 500 vya kutoa mafunzo ya udereva kutuma maombi ya leseni mpya kwa lengo la kunasa vyuo feki na wakufunzi ambao hawajahitimu.

Vyuo vingi vya mafunzo ya udereva vimesheheni wakufunzi ambao hawajahitimu na hawajatimiza matakwa yaliyowekwa na NTSA.

Chama cha Wamiliki wa Vyuo vya Mafunzo ya Udereva (KDSA) kimeenda kortini kwa mara nyingine katika juhudi za kutaka kuzuia NTSA kuvitaka kutuma upya maombi ya leseni.

Kwenye malalamishi yake, KDSA inadai kwamba ina jumla ya wanachama 700, ambapo vyuo vyao viko kwenye hatari ya kufungwa ikiwa masharti hayo mapya ya NTSA yatatekelezwa.

Chama hicho kinaongozwa na Bw Samuel Kariuki.

Chini ya masharti hayo mapya, NTSA inalenga kuwatuma maafisa wake kukagua vyuo hivyo kuhakikisha vimetimiza masharti yote kuhusu miundomsingi bora na wafanyakazi waliohitimu. Ni baada tu ya kutimiza viwango hivyo ambapo vitapewa leseni mpya.

Miongoni mwa miundomsingi ambayo lazima viwe navyo ni maeneo ya watu kungoja kuhudumiwa, afisi za wasimamizi wake na madarasa ya kuwafunzia wanaojifunza udereva.

Kulingana na masharti hayo, ni lazima kila darasa liwe na nafasi ya kuwatoshea wanafunzi wanne huku wakiwa wametengana kwa umbali wa mita moja.

Vile vile, lazima viwe na vyoo na alama za barabarani zilizoidhinishwa na mamlaka hiyo.

Walimu watahitajika kuwa angaa wamefikisha alama ya D- kwenye Mtihani wa Kidato cha Nne (KCSE).

Vyuo hivyo pia lazima viwasilishe ripoti maalum kwa NTSA kila Januari mwaka unapoanza.

You can share this post!

Aina mpya hatari ya corona yagundulika

Barcelona na Boca Juniors kupimana ubabe kwenye kipute...

T L