• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
Abiria 4 waaga dunia, tisa wajeruhiwa kwenye shambulio Mandera

Abiria 4 waaga dunia, tisa wajeruhiwa kwenye shambulio Mandera

NA MANASE OTSIALO 

WATU wanne wameaga dunia baada ya matatu kukanyaga kilipuzi eneo la Qurqura katika barabara ya Mandera-Elwak, Naibu Kamishna wa Mandera Kusini Tobias Otunga amethibitisha.

“Saa tano asubuhi tumepata ripoti kwamba matatu iliyokuwa ikielekea Elwak kutoka Mandera ilikuwa imegongwa na kilipuzi. Abiria wanne wamepoteza maisha na tisa wamejeruhiwa na kwa sasa wanapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Elwak,” amesema Bw Otunga kwa simu.

Tayari maafisa wameanzisha msako kuwatafuta waliotekeleza shambulio hilo.

“Tunashuku kwamba kilipuzi kilitegwa ardhini na Al-Shabaab waliolenga magari ya maafisa wa usalama na watumiaji wengine wa barabara,” amesema.

Shambulio hilo ni la pili kutokea mwezi huu wa Septemba.

Mnamo Septemba 3, 2023, polisi wawili waliangamia baada ya gari lao kulengwa na kilipuzi walipokuwa wakitoka eneo la Arabia kuelekea mjini Mandera.

Polisi hao walikuwa wanaenda kuomba lifti kwenye gari jingine la polisi lililokuwa linaelekea jijini Nairobi.

Maafisa hao walikuwa wanaanza likizo yao walipokumbana na kifo.

  • Tags

You can share this post!

Wanahabari wafukuzwa wakifuatilia stori ya moto shuleni...

Liverpool watoka nyuma na kuendeleza masaibu ya Wolves...

T L