• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Mahakama yaagiza Rotich ashtakiwe upya

Mahakama yaagiza Rotich ashtakiwe upya

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Waziri wa Hazina Kuu ya Kitaifa Henry Rotich alipata pigo kubwa Jumatatu mahakama ya kesi za ufisadi ilipoamuru kesi za kashfa ya Sh63 bilioni za mabwawa ya Arror na Kimwarer ziunganishwe.

Kesi hizo ni ile Bw Rotich na ile ya kinara wa mamlaka ya kustawisha bonde la Kerio Bw David Kipchumba Kimosop.

Hakimu mkuu Bw Lawrence Mugambi alitupilia mbali ombi la Bw Rotich aliyeomba mahakama ikatae ombi la Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma (DPP) na kuamuru kesi aliyoshtakiwa iendelee kivyake.

Bw Mugambi alikubalia ombi la DPP la kuunganishwa kwa kesi hiyo na mashtaka kupungwa hadi 30 na mashahidi kupunguzwa kutoka 104 hadi 52.

Idadi ya washtakiwa ilipunguzwa kutoka 30 hadi watu tisa.

Sasa mashtaka mapya aliyowasilisha DPP kupitia kwa viongozi wa mashtaka Bw Taib Ali Taib na naibu wa DPP Alexander Muteti yataendelea.

Bw Rotich ameshtakiwa pamoja na Bw Kimosop, Kennedy Nyakundi Nyachiro,Jackson Njau Kinyanjui, ,William KiPkemboi Maina, Paul Kipkoech Serem, Francis Chepkonga Kipkech, Titus Muriithi na Geoffrey Mwangi Wahungu.

Washtakiwa hao tisa walikana shtaka la kufuja pesa za serikali zenye thamani ya dola za Kimarekani USD 501,829,769.

Shtaka lilisema washtakiwa hao walitia saini kandarasi na kampuni za Italia wajenge mabwawa hayo bila kufuata sheria na mwongozo wa serikali.

Huku mahakama ikiruhusu washtakiwa wasomewe mashtaka upya, mawakili Katwa Kigen na Kioko Kilukumi waliomba mahakama itupilie mbali kesi hiyo inayowakabili washtakiwa wakidai imekawia mahakamani kwa zaidi ya miezi 24 tangu washikwe na kushtakiwa.

Mawakili hao walisema chini ya sheria za kupambana ufisadi kesi hizo zinafaa kukamilika katika muda wa miaka miwili.

Washtakiwa hao walikanusha mashtaka 30 mapya na kesi inayowakabili itaanza kusikilizwa mnamo Novemba 23, 2021.

  • Tags

You can share this post!

Matiang’i ajibu madai ya wandani wa Dkt Ruto kuhusu...

Vinyago wa Uhuru

T L