• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 11:02 AM
Akothee ajibu mashabiki wake kuhusu uraia wa Omosh

Akothee ajibu mashabiki wake kuhusu uraia wa Omosh

Na FRIDAH OKACHI

MWANAMUZIKI na mfanyabiashara Esther Akoth almaarufu Akothee amekana madai kuwa mumewe anayeaminika kuwa kwenye mgogoro naye, kuwa si raia wa Pakistan.

Kupitia video ya moja kwa moja katika ukurasa wake wa Facebook, Akothee anasema Denis Schweizer almaarufu Omosh, si raia wa Pakistan bali ni kakaye ambaye anaishi nchini humo.

Akothee alijibu kwa ufasaha na kusisitiza kuwa Bw Schweizer anatoka taifa la Uswizi.

Mfanyabiashara huyo amewakejeli mashabiki wake kwa kukosa kibali cha kusafiri.

“Wengine wenu mnasema Omosh hatoki Uswizi? Mnapayuka ilhali hamna paspoti ya usafiri. Hata hamjawahi tembelea afisi za uhamiaji,” alisema Bi Akothee.

Mama huyo wa watoto watano waliwambia mahasidi wake wanaomfuatilia, wanaoishi Pakistan ni watu.

Katika mtandao wa WhatsApp, Bi Akothee ambaye ana umri wa miaka 43 amechapisha picha kadhaa akiwa shambani akiwa na mmoja wa wafanyakazi wake wakivuna malenge.

Picha moja ikiwa na ujumbe kwa lugha ya Dholuo, “see the budho of Omosh. Omosh to Lweteber.” Ujumbe huo ukiwa na maana yake kuwa tazama malenge ya Omosh. Omosh ana mikono ya kazi nzuri. Ujumbe huu ukiwa na ishara kuwa bado wapo pamoja kwenye mahusiano.

Siku za hivi karibuni, mwanamziki huyo alichapisha taarifa ndefu kuhusu hali yake na kushukuru marafiki wake wa karibu haswa Nelly Oaks ambaye alisema amekuwa wa msaada mkubwa.

Kumekuwepo na madai kwenye mitandao ya kijamii kwamba Omosh si mzaliwa wa taifa la Uswizi ila ni mwigizaji wa Kipakistani ambaye familia yake ipo nchini Pakistan.

  • Tags

You can share this post!

Maswali yaibuka Kipchoge kukawia kupongeza chipukizi...

Mademu wanikataa sababu naogelea usiku kucha bila kufika...

T L