• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Aliyejifanya askari na kutapeli dereva kizimbani

Aliyejifanya askari na kutapeli dereva kizimbani

Na RICHARD MUNGUTI

TAPELI aliyejifanya polisi na kupora dereva wa teksi simu na Sh1, 300 kabla ya kuchana mbuga amefikishwa kortini.

Joshua Barongo mwenye ujanja wa sungura alimuomba simu Daniel Mutua ndani ya kituo cha polisi cha Embakasi ampigie mwenzake lakini akatorokea mlango wa nyuma.

Barongo alikuwa ameabiri gari la Mutua kutoka Athi River kuelekea Embakasi.

Mshukiwa huyo alikuwa amesikizana na Mutua atamlipa Sh1, 300 kwa safari hiyo.

Walipofika kituoni, Barongo alimwacha Mutua akaingia ndani kisha akachomoka akipitia mlango wa nyuma.

Aliabiri bodaboda na kutoroka. Mutua naye alimwandama kwa piki piki.

Alimshikwa na kupata simu yake.

Mlalamishi alishangaa jinsi alijifanya kuwa afisa wa polisi, akiwa ndani ya kituo cha polisi cha Embakasi.

Mshtakiwa alikabiliwa na shtaka la wizi wa simu ya Sh17, 000 na pesa tasilimu Sh1, 000.

Alikana mashtaka mbele ya hakimu mkuu Francis Kyambia.

Barongo alikiri shtaka la kutoroka na simu na kuzuiliwa katika gereza la viwandani kusibiri adhabu.

  • Tags

You can share this post!

Polisi Juja wakatazwa kuuza pombe

Ezekiel Odero atua jijini Nairobi kuhubiri injili

T L