• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Aliyetumia majina mawili tofauti ajipata taabani ujenzi wa majumba ukisitishwa

Aliyetumia majina mawili tofauti ajipata taabani ujenzi wa majumba ukisitishwa

NA RICHARD MUNGUTI

UJENZI wa majumba ya orofa 18 kila moja katika ardhi ya umma ya ekari 40.7 umesimamishwa baada ya Mahakama Kuu kuelezwa mstawishaji alinyakua kipande hicho akitumia majina mawili tofauti.

Mbali na majina mawili, Jaji Edward Wabwoto alielezwa mwekezaji huyo Ubdi Yahye Hagi alitumia kitambulisho cha Duncan Ng’ang’a Kimani kuomba hatimiliki katika Wizara ya Ardhi.

Akiomba Wizara ya Ardhi impe hatimiliki, Ubdi alimkabidhi kamishna wa ardhi kitambulisho nambari 3042617.

Uchunguzi uliofanywa na mawakili Byran Khaemba na Ben Nzakyo wanaowakilisha wapangaji 5,000 wa mtaa wa Juja Road Estate waligudua kitambulisho hicho kilikuwa kimepewa Bw Duncan Ng’ang’a Kimani.

Mawakili hao walimfichulia Jaji Wabwoto kwamba mwekezaji huyo anatumia majina Ubdi Yahye Hagi na Udbi Yahye Haji.

Katika afisi ya Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Nchini (KRA), Ubdi alijitambua kuwa mwenye kitambulisho nambari 3042617 (cha Kimani).

Katika ushahidi aliotoa mahakamani Ubdi amesema kitambulisho chake ni nambari 2790124.

Lakini alipomuuzia Muhyidin Mohamed Dhuhulow sehemu ya shamba hilo la umma lililotengwa kwa ujenzi wa zahanati na shule ya umma,Ubdi aliandika katika hatimiliki kwamba kitambulisho chake ni nambari 3042617.

Katika afidaviti aliyowasilisha kortini, Ubdi amesema jina lake ni Ubdi Yahye Hagi lakini katika hati za mauzo kwa Dhuhulow alisema jina lake ni Udbi Yahye Haji.

Mahakama ilifahamishwa mlalamishi alisema katika cheti cha PIN ya KRA alizaliwa mnamo 1958 katika Kaunti ya Mandera.

Katika afidaviti nyingine aliyowasilisha kortini, Ubdi anadai alizaliwa Januari 1, 1968 katika wilaya ya Isiolo.

Mandera na Isiolo ziko na umbali wa kilomita 900.

Mahakama ilielezwa na wakili wa Serikali Allan Kamau kwamba atawasilisha ushahidi kuthibitisha ardhi inayong’ang’aniwa ni ya umma.

Jaji Wabwoto aliamuru kesi hiyo itaendelea Julai 20, 2023.

Kwa sasa mahakama iliamuru ujenzi huo usimamishwe.

  • Tags

You can share this post!

Tuwei amezea mate kiti cha naibu rais wa Shirkisho la...

West Ham watibua jaribio la kwanza la Arsenal kumsajili...

T L