• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Tuwei amezea mate kiti cha naibu rais wa Shirkisho la Riadha Duniani

Tuwei amezea mate kiti cha naibu rais wa Shirkisho la Riadha Duniani

Na GEOFFREY ANENE

MWENYEKITI wa Shirikisho la Riadha Kenya (AK) Jackson Tuwei alitangaza mnamo Juni 15 kwamba anajitosa kwa kinyang’anyiro cha kuchaguliwa kuwa naibu rais wa Shirikisho la Riadha Duniani (WA).

Tuwei atawania mojawapo ya nyadhifa nne za manaibu rais wa shirikisho hilo lenye wanachama 214 mnamo Agosti 17.

Wagombea wengine ni Nawaf Bin Mhammed Al Saud (Saudi Arabia), Raul Chapado (Uhispania), Abby Hoffman (Canada), Antti Pihlakoski (Finland), Ximena Restrepo (Chile), Adille Sumariwalla (India) na Geoff Gardner (Kisiwa cha Norfolk).

Tuwei pia analenga mojawapo ya viti 13 vya wajumbe. Kitengo hiki kimevutia wawaniaji 26 wakiwemo pia Waafrika Beatrice Ayikoru (Uganda), Nawal El Moutawakel (Morocco), James Moloi (Afrika Kusini).

Wadhifa wa rais wa Shirikisho la Riadha Duniani, ambao unashikiliwa na Sebastian Coe, umevutia Muingereza huyo pekee kumaanisha ataingia bila kupingwa.

Tuwei aliyetumikia taifa kama mwanajeshi kwa miaka 39 kabla ya kustaafu mwaka 2010 amehudumu kama naibu rais wa Shirikisho la Riadha Afrika (CAA), eneo la Afrika Mashariki na mwenyekiti wa riadha za majeshi Afrika Mashariki.

  • Tags

You can share this post!

Idadi ya watu waliothibitishwa kufariki Shakahola yagonga...

Aliyetumia majina mawili tofauti ajipata taabani ujenzi wa...

T L