• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 6:50 AM
Afueni kwa wakazi wa Gatuanyaga barabara ikianza kujengwa

Afueni kwa wakazi wa Gatuanyaga barabara ikianza kujengwa

Na LAWRENCE ONGARO

WAKAZI wa Gatuanyaga, Kaunti ya Kiambu wamepata afueni kutokana na ujenzi wa barabara ya Munyu-Gatuanyaga hadi Kang’oki mjini Thika.

Barabara hiyo itagharimu takribani Sh1 bilioni.

Wakazi wa Gatuanyaga na vitongoji vyake wametaja mradi huo kama wa kipekee kwa sababu kwa miaka mingi hawajapata barabara ya lami.

Bw Joseph Kaveri ambaye ni mkazi wa Gatuanyaga alisema anaamini kwamba mradi huo wa barabara utaleta mabadiliko makubwa kimaendeleo ambapo biashara zitaimarika.

Mradi huo unaendeshwa na serikali kuu kwa ushirikiano na serikali ya Kaunti ya Kiambu.

Bw Kaveri alisema msimu wa mvua wakazi wa eneo hilo hupata changamoto tele kwa sababu usafiri huwa shida.

“Malori ya kubeba mawe na wahudumu wa bodaboda ndio huathirika zaidi. Kwa hivyo, kero itaisha barabara hiyo itapokuwa imekamilika,” alifafanua mkazi huyo.

Naye Bw Benson Muyu ambaye ni mfanyabiashara wa eneo hilo anasema kuwa wakati wa mvua biashara nyingi hukwama kwa sababu ya ubovu wa barabara.

Kulingana na kaunti ya Kiambu barabara hiyo ni ya umbali wa kilomita 17 ambapo italeta afueni kwa wakazi wa eneo hilo.

Alisema mara nyingi mvua ikinyesha wao hulazimika kuzunguka mwendo wa zaidi ya kilomita nane hivi ili kufika katika mji wa Thika.

“Hata wafanyabiashara wengi wa chakula watapata afueni wakienda katika soko la Madaraka, Makongeni, Thika kununua vyakula hivyo.” akasema Bw Muyu.

Katika siku za hivi karibuni watu wengi wamehamishwa katika eneo hilo kupisha miradi ya maendeleo huko.

  • Tags

You can share this post!

Lori la polisi lagonga nyumba za mtaa wa mabanda

Watu 10,000 pekee kuhudhuria sherehe za Mashujaa Kirinyaga