• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Broadway yawapa wakongwe na watoto chakula wajienjoi

Broadway yawapa wakongwe na watoto chakula wajienjoi

NA LAWRENCE ONGARO

WAKAZI wa kijiji cha Kiganjo mjini Thika mnamo Jumamosi walianza kuonja vitamu vya sikukuu ya Krismasi baada ya kufadhiliwa na kampuni ya Broadway ambayo huoka mkate.

Krismasi imeadhimishwa rasmi leo Jumapili.

Wakongwe na watoto walipewa mikate na soda na vyakula vingine tofauti.

Mkurugenzi wa kampuni ya Broadway Bimal Shah, aliandamana na MCA wa wadi ya  Kamenu – Thika, Peter Mburu huku wakipeana chakula cha Krismasi.

Wengine walioandamana nao ni aliyekuwa MCA wa Kamenu Elizabeth Muthoni Hussein na DJ Mo akiwa pamoja na mkewe ambaye ni Size 8.

Bw Shah alisema kuna haja ya kuwajali wasiojiweza na kwa hivyo wakongwe na watoto wanastahili kunufaika.

Bw Shah na MCA wa Kamenu Bw Mburu waliwafaa pakubwa wakazi wa Kiganjo na vitongoji vyake.

“Msaada wa aina hii hutolewa kila mara na kwa hivyo mwezi huu wa Desemba ni muhimu kwetu kuwasaidia wasiojiweza,” alisema Bw Shah.

Kampuni  ya Broadway imekuwa kwenye biashara kwa zaidi ya miaka 60 na imekuwa ikitoa misaada kwa wasiojiweza katika makazi duni mjini Thika kama Kiandutu, Athena, na Madharau.

Broadway yawapa wakongwe na watoto chakula wajienjoi. PICHA | LAWRENCE ONGARO

Bw Mburu alisema amelazimika kujumuika na wakazi wa Kiganjo ili wapate msaada wa chakula.

“Nililazimika kushirikiana na kampuni ya Broadway ili niwasaidie watu wangu ninaowawakilisha. Wakongwe na watoto hasa ndio walinufaika na misaada hiyo,” alisema Bw Mburu.

Alisema atahakikisha wakazi wa Kamenu hawapati shida kwani anafanya juhudi wakazi hao wapate maji ambayo yamekuwa adimu kwao kuyapata.

“Tayari nitafanya juhudi kuona ya kwamba ahadi zote nilizowaahidi zinatekelezwa ipasavyo,” alijitetea MCA Mburu.

Alisema wakati wa hafla hiyo ya Jumamosi wakongwe wapatao 120 na watoto 100 walipokea msaada wa chakula ili washerehekee sikukuu ya Krisimasi kwa furaha.

“Tumejadiliana na kampuni ya Broadway na kuafikiana kuwa kila mara tutakuwa tukiwatembelea wasiojiweza ili wapate misaada,” alisema kiongozi huyo.

  • Tags

You can share this post!

JAMVI LA SIASA: Uasi mpya watishia kuvuruga ODM

Chebukati asema hajuti anapoondoka afisini Januari 17, 2023

T L