• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Bunge la Vihiga kujadili iwapo mawaziri wanne watimuliwe au la

Bunge la Vihiga kujadili iwapo mawaziri wanne watimuliwe au la

Na DERICK LUVEGA

MJADALA kuhusu hoja za kutimuliwa kwa mawaziri wa kaunti na kampeni ya kusimamishwa kwa serikali ya Kaunti ya Vihiga ni masuala ambayo yatateka hisia za madiwani leo Alhamisi watakaporejelea vikao baada ya likizo fupi.

Naibu Spika Zacharia Murefu alisema Bunge hilo litatumia kikao hicho kubuni kama teule itakayochunguza mawaziri ambao walitimuliwa kwa lengo la kuidhinisha kuondolewa kwao.

Hoja za kuondolewa afisini kwa mawaziri Pamela Kimwele (Utumishi wa Umma), Amos Kutwa (Afya), Paul Mbuni (Ardhi) na Kenneth Keseko (Biashara) zilipitishwa kwenye kikao maalum cha bunge hilo mnamo Mei 27.

Hatua hiyo hata hivyo, ililaaniwa na viongozi wa makundi ya kutetea haki ya kijamii katika kaunti ya Vihiga ambao walisema italemaza shughuli katika serikali hiyo.

Kulingana na Spika Murefu, kamati hiyo teule itapewa muda wa siku saba ambapo itawaita mawaziri hao wanne na kuwahoji zaidi kabla ya kuwasilisha ripoti yake katika bunge hilo la Vihiga lenye madiwani 38.

Ikiwa bunge hilo litaidhinisha kutimuiwa kwa mawaziri hao, Gavana wa Vihiga Wilbur Otichillo atakuwa huru kuwafuta kazi rasmi.

Mawaziri hao wanne wamekashifiwa kwa makosa ya utepetevu kazini, matumizi mabaya ya afisi zao na ukiukaji wa Katiba.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

You can share this post!

Wanafunzi wa kike kunufaika na ufadhili wa sodo

Washukiwa 12 wa genge la Wakali Kwanza wajisalimisha